Articles by "MIKOANI"
Showing posts with label MIKOANI. Show all posts
Na Mwandishi Wetu.

Wakati zoezi la uhakiki, usasishaji na usajili wa Anwani za Makazi likiendelea katika Halmashauri sita za Mkoa wa Arusha, Halmashauri ya Monduli imefanikiwa kufikia asilimia 22.77 ya usasishaji anwani za makazi ndani ya siku 5 kutoka Agosti 17 hadi  21 mwaka huu 2024.

Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo ofisini kwake tarehe 21  Agosti, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi Happiness Laizer, amesema Anwani zilizosasishwa hadi leo mchana ni  6621 kati ya 29,082 zilizosajiliwa mwaka 2022.

Bi. Laizer amesema anwani mpya zilizosajiliwa ni 1,358 sawa na ongezeko la asilimia 4.67 yakiwa ni mafanikio makubwa kwa eneo hilo linalokaliwa na jamii ya Kimasai.

Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Laizer, tarehe 21 Agosti, 2024.

Pamoja na mambo mengine wamezungumzia zoezi la Uhakiki, Usasishaji wa Anwani za Makazi na Usajili wa Anwani mpya linaloendelea pamoja na matumizi ya Mfumo wa programu Tumizi ya NaPA na huduma ya Barua ya Utambulisho Kidigitali.

Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea Kaburi la Hayati Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Nne lililopo nyumbani kwake Kijiji cha Ngarashi, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. 

Timu hiyo ya wataalamu ikifika katika makazi ya kiongozi huyo wakati wa zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi linaloendelea katika kijiji hicho tarehe 21 Agosti, 2024.
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Moringe Sokoine yaliyopo katika Kata ya Monduli Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. 

Wataalam hao walipata nafasi hiyo wakati wakikagua maendeleo ya zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi ambapo walipata nafasi ya kutembelea Kaburi la Kiongozi huyo lililopo nyumbani kwake tarehe 21 Agosti, 2024.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo Januari 23, 2024 amefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayoendelea katika mkoa wake wilayani Babati.

Ziara hiyo ilianzia katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) katika Hospitali ya Mji wa Babati, ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kujitahidi ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa haraka.

Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Mji Daktari Kyabaroti Kyabaroti amesema kuwa jengo hilo lilitengewa Mil. 300 ambapo mpaka sasa lipo katika hatua za umaliziaji na ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa Februari litaanza kutumika.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiteta jambo na Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini.
Pia, Mhe. Queen Sendiga alipata wasaa wa kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini ulioanza Oktoba 25, 2023.

Mhe. Sendiga amejionea ujenzi huo huku akiwataka wataalamu hao kumaliza kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote vitavyosababisha ukwamishaji wa ujenzi huo.

Ujenzi huo unaogharimu shilingi Mil. 600 ambapo awamu ya kwanza wamepewa zaidi ya mil. 285 kwa ajili ya ukamilishaji wa Boma, msingi mpaka gorofa ya kwanza na sasa ujenzi umefikia asilimia 21.4.

Aidha Jeshi la Zimamoto Walimemshukuru Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwezesha majeshi ya Tanzania katika kukabiliana na majanga mbali mbali huku wakimshukuru Mhe. Sendiga na ofisi yake kwa ujumla kuweza kuwawezesha katika miongozo mbali mbali.
Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati. 
Baadae Mhe. Queen Sendiga alifika katika mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati. Mradi ulibuliwa baada ya Serikali kuanzisha mkoa wa Manyara mwaka 2002 na ndipo uhitaji wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa ulipotokea.

Jengo hilo la ghorafa nne ambapo likikamilika litakuwa na jumla ya vyumba vya ofisi 33 kati ya hivyo 06 ni vyumba vya ofisi za maafisa wakuu ngazi ya mkoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema utekelezaji unaoendelea ni awamu ya Kwanza ambayo ilianza baada ya Serikali kutoa fedha mnamo mwezi Aprili 2023 jumla ya shilingi milioni mia nane tu (TShs.800,000,000.00) ambazo zilipokelewa Polisi Mkoa Manyara.

Amesema kazi zilizofanyika ni ujenzi wa msingi, nguzo na sakafu za ghorofa zote nne huku wakifanya maandalizi ya ujenzi wa kuta za pamoja na kuezeka na ujenzi wa chumba cha mitambo ya lifti ambapo wanatarajia ujenzi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari.

Nae Mhe. Sendiga amewapongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kutekeleza mradi kwa vitendo huku akizitaka taasisi nyingine zenye miradi mkoani humo kuiga Jeshi la Polisi.

Aidha Mhe. Sendiga amemtaka mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kuhakikisha anasimamia kwa ufasaha ujenzi wa jengo la ofisi ya yake linakamilika kwa wakati maana ujenzi wake umekuwa ukisua sua jambo linaloleta ukakasi kila anapotembelea.

Jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Babati ambapo ujenzi wake umekuwa ukisua sua. (Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara)
Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bw. Kennedy Ntenje (wa tatu kulia) akiwa ameshikilia mfano wa hundi pamoja na Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake iliyofikia tamati wateja walikuwa na fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) pamoja na Mkuu wa Kanda Nyanda za Juu Kusini - Vodacom Tanzania, Abednego Mhagama (wa kwanza kushoto) wakikabidhi mfano wa kadi ya bima kwa Kaimu Mganga Mfawidhi, Dkt. Scholastica Malangalila na mmojawapo wa akina mama walionufaika, Bi. Grace John (katikati) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake iliyofikia tamati ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu uliomalizika.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) akifurahia pamoja na mmojawapo wa akina mama na mtoto wake walionufaika na bima ya bure ya afya kutoka Vodacom Tanzania, Bi. Grace John katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake iliyofikia kikomo ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu uliomalizika.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC mara baada ya kukabidhi bima kubwa za bure kwa akina mama na mtoto wao kwa mwaka mzima katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake iliyofikia kikomo ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu uliomalizika.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa pamoja na mshindi wa luninga kupitia kampeni iliyofika kikomo ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hiyo wateja walikuwa na fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa pamoja na mshindi wa pikipiki kupitia kampeni iliyofika kikomo ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hiyo wateja walikuwa na fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa pamoja na mshindi wa simujanja kupitia kampeni iliyofika kikomo ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hiyo wateja walikuwa na fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Msanii wa Bongo Flava maarufu kama ‘Dogo Janja’ akijumuika pamoja na wakazi wa Iringa kutoa burudano kupitia kampeni iliyofika kikomo ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’ ya Vodacom Tanzania PLC, katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mkoani humo mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hiyo wateja walikuwa na fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe kulia akimgaia mche wa Mbegu ya Mchikichi zinazozalishwa na Shamba la Wakala wa Mbegu Asa Mkinga Mkulima wakati wa halfa ya ugawaji miche hiyo shamba la Mwele lililopo wilaya ya MkingaWAZIRI wa Kilimo Husein Bashe katika akionyeshwa maeneo mbalimbali yeye miche ya Michikichi kwenye Shamba la Wakala wa Mbegu Asa lililopo wilayani Mkinga wakati wa ziara yake kulia ni Mtendaji Mkuu wa Asa Sophia Kashenge na kushoto ni mkulima aliyepewa miche shamba la Mwele lililopo wilaya ya Mkinga
Waziri wa Kilimo Husein Bashe katikati akitembelea Shamba la Wakala wa Mbegu ASA wilaya ya Mkinga wakati wa ziara yake shamba la Mwele lililopo wilaya ya Mkinga kulia ni Mtendaji Mkuu wa ASA Sophia Kashenge akisisitiza jambo
Mtendaji mkuu wa wakala wa Mbegu (ASA) Sophia Kashenge kushoto akimueleza jambo Waziri wa Kilimo Husein Bashe wakati alipotembelea wakala huo kwa ajili kugawa miche kwa wakulima
Mtendaji mkuu wa wakala wa Mbegu (ASA) Sophia Kashenge wa pili kutoka kulia akimuonyesha kitu Waziri wa Kilimo Husein Bashe wakati wa ziara yake kwenye Shamba hilo
Waziri wa Kilimo Husein Bashe akizungumza na wakulima wa wilaya ya Mkinga wakati wa ziara yake ya kutembelea Shamba la Mwele lililopo wilayani Mkinga
Mkurugenzi wa Bodi Mkonge Tanzania (TSB) Saady Kambona akiwa na viongozi wengine wakifuatilia kwa umakini maelekezo ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Watumishi wa Wakala wa mbegu za kilimo nchini (ASA) katika shamba la Mwele lililopo wilaya ya Mkinga wakiwa na viongozi wengine wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Kilimo Husein Bashe

Na Oscar Assenga,MKINGA

WAKALA wa mbegu za kilimo nchini (ASA) katika shamba la Mwele lililopo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wamezindua zoezi la ugawaji wa mbegu za michikichi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kutaka zao hilo litumike ipasavyo kuongeza uzalishaji wa mafuta hapa nchini.

Hatua ya utekelezaji huo imekuwa na mafanikio makubwa naa kwa sasa wana michikichi elfu 88 na lengo ni kutoa michikichi laki mbili kwa wakulima ambao wataipanda katika maeneo mbalimbali na hivyo kuwezesha kilimo cha zao kuwa na tija

Akizungumza wakati akikabidhi Miche ya Michikichi kwa Wakulima wwa zao hilo lengo likiwa ni kukabidhi michikichi laki mbili katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga,Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema wananchi wanaopewa miche hiyo lazima wajaze fomu na kusaini ikiwemo kubaki na kumbukumbu ambazo zitapelekewa Halmashauri.

Alisema zitapelekwa huko ili maafisa kilimo wapewe taarifa kwenye vijiji vyao ambavyo wananchi wamepewa miche ili wawafuatilie kwa ukaribu wanapopata matatizo waone namna ya kuyapatia ufumbuzi huko huko vijijini.

Waziri Bashe alisema kwa sababu wamekuwa bahati mbaya wakigawa miche lakini mingi inaishia njiani haikui na wananchi wanapoteza muda na kuweka nguvu zao hivyo ni muhimu uwepo wa ufuatiliaji huo

“Leo tunagawa miche ya Michikichi wilaya ya Mkinga na wananchi ambao wamepewa watajaza fomu kusaini na kubaki na kumbukumbu ambazo baadae zitapelekwa Halmashauri pia maafisa Kilimo wapewa Taarufa kwenye Vijiji vyao kwa lengo la kuwa na ufuatiliaji wa karibu watakakukumbana na matatizo waweze kuyapatia ufumbuzi”Alisema

Hata hivyo Waziri huyo alisema wataanzisha mashamba makubwa ya pamoja ambao amesema miongoni mwa wafaidika watakuwa wananchi wa maeneo husika huku akisisitiza umuhimu wa maafisa kilimo wakae vijijini.

“Kama walimu wanakaa vijijini na maafisa kilimo nao wakate vijiji lakini pia mikutano ya Serikali za vijiji ifanye kazi ya kujadili maafisa Kilimo maeneo hayo kama hawatimizi wajibu wao kama hawafanyi hivyo serikali za vijiji ziandike taarifa kwenye mustasari zipelekewe kwenye WDC halafu ziende Halmshauri”Alisema

Waziri huyo alisema kwamba katikaa taarifa hiyo waeleze Afisa kilimo walionae hajawahi kuwatembelea wakulima hata siku moja kwani Serikali imegawa pikipiki na sasa wanawapa vishkambie na wamepekea vipima afya vya udongo ili wanapopima shamba wawaambie kama shamba linafaa kulima mashina au na huduma hiyo ni bure.

Katika hatua nyengine Waziri Bashe amemuagiza Mkurugenzi wa Asa Sophia Kashenge waanze shughuli za kuzalisha miche ya minazi kwenye kituo hichgo kama wanavyozalisha mice ya mazao mengine ili wananchi waweze kupata m iche ya minazi kutoka kwenye kituo hicho,

Awali akizungumza katika Mtendaji mkuu wa wakala wa Mbegu (ASA) Sophia Kashenge alisema kwa sasa wana michikichi elfu 88 na lengo ni kutoa michikichi laki mbili kwa wakulima.

Sophia alisema kwamba wamefarijika sana kuona Waziri kufika katika shamba hilo ambalo kipindi cha nyuma lilikuwa limetekelezwa lakini nguvu ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu imeonekana na wameweza kulifufua.

Alisema kwamba huwezi kufanya uzalishaji bila kuwa na miuondombinu ya umwagiliaji na hivyo lengo lao wataendelea kuongeza uzalishaji wa mbegu jambo ambalo ni kipaumbele cha nchi.

“Suala la Uzalishaji wa Mbegu za Michikichi ni Agizo la Waziri Mkuu tokea 2018 na sisi tumeitika vizuri tuna mashamba matatu ya ASA na la Mkinga ni la pili kwa uzalishaji wa michikichi na tunaamini kazi tunayoifanya ni kumuongezea mwananchi kipato”Alisema

Naye kwa upande wake Mkulima wa zao la Michikichi Mtarajiwa wilayani Mkinga Maaono Mkangwa alisema serikasli imechukua uamuzi mzuri kuwaletea kilimo hicho ambacho wanaamani kitawainua kiuchumi.

Mpango wa serikali ni kupunguza kiwango kikubwa cha kuingiza mafuta kutoka nje ya nchi wakati mafuta hayo yanaweza kuzalishwa na wakulima hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ranchi ya Mbogo Bw. Naweed Mullah (kulia) akimuongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi (kushoto) na timu ya washiriki wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula (AGRF) waliofika shambani kwake Chalinze, Septemba 03,2023 kwa ajili ya kuona namna anavyofanya shughuli zake.
Meneja Uendelezaji biashara kutoka kiwanda cha kusindika nyama cha "TANCHOICE" Bw. Luwungo Hassan (aliyesimama mbele) akielezea kwa ufupi historia ya kiwanda hicho kwa washiriki wa Mkutano wa Jukwa la mifumo ya Chakula (AGRF) waliofika kiwandani hapo Septemba 03, 2023.
Sehemu ya aina ya Ng'ombe waliopo kwenye ranchi ya Mbogo iliyopo Chalinze mkoani Pwani.

Nchi za China na Kenya zimeonekana kuvutiwa na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya Mifugo mara baada ya kuwatembelea wawekezaji wa ndani ambao ni Ranchi ya Mbogo na Kiwanda cha kuchakata nyama cha “Tanchoice” vilivyopo mkoani Pwani Septemba 03, 2023.

Ziara hiyo ambayo ni miongoni mwa shughuli za utangulizi zinazofanyika kabla ya kufanyika kwa mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula barani Afrika (AGRF) iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi ambapo alibainisha kuwa Wizara yake imejiandaa kikamilifu kutumia fursa zitakazojitokeza katika pindi chote cha mkutano huo kuiimarisha sekta ya Mifugo nchini.

“Sisi kwa sasa kama nchi tunasema “flagship” ya wizara yetu ni nyama na samaki ambazo tunazipeleka nje ya nchi na kwa mwaka jana tulifanikiwa kusafirisha tani elfu 14 na malengo yetu ni kuvuka tani elfu 16 kwa mwaka huu wa fedha na hilo tunaweza kufanikiwa kwa kuleta wadau wengi zaidi kama mbogo ranchi” Amesema Dkt. Mushi.

Aidha Dkt. Mushi ameongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kupata wawekezaji na masoko mapya ili nyama inayozalishwa nchini iweze kuuzwa kwa wingi nje ya nchi hatua ambayo anaamini itachangia ongezeko la fedha za kigeni kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ranchi ya Mbogo Bw. Naweed Mullah amesema kuwa anatarajia kutumia mkutano huo wa kimataifa wa jukwaa la Mifumo ya chakula kuhakikisha anatoa elimu ya kutosha kwa washiriki wa ndani na nje ya nchi kuhusu njia bora za uongezaji thamani wa ng;ombe wa asili waliopo hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla.

“Tunajua ulimwengu mzima unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula hasa nyama na hali ya upatikanaji wa zao hilo imeendelea kushuka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo tunaamini jukwaa hili limelenga kujadili namna bora ya kukabiliana na changamoto hiyo” Ameongeza Bw. Mulllah.

Naye mmoja wa washiriki wa ziara hiyo Bi. Wangari Kurya kutoka nchini Kenya mbali na kukoshwa na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta ya Mifugo nchini amevutiwa zaidi na namna Serikali inavyohamasisha aina zote za kilimo ikiwa ni tofauti na kwao ambako kilimo mazao ndio kimekuwa kikisisitizwa zaidi.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya “FAMSUN” kutoka nchini China Bw. Joy Lee amevutiwa na namna Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na ardhi kubwa na nzuri kwa ajili ya kufanya shughuli za ufugaji tofauti na hali ilivyo nchini kwao ambako wanalazimika kutumia kiwango kikubwa cha teknolojia ili kutekeleza shughuli hizo kwenye maeneo madogo waliyonayo.

“Ninatoa wito kwa wawekezaji wote kuja Tanzania kuna fursa nyingi sana za uwekezaji kwa upande wa sekta ya Mifugo” Amehitimisha Bw. 

Mkutano wa Jukwaa la kujadili Mifumo ya chakula barani Afrika unatarajiwa kufanyika hapa nchini kuanzia Septemba 05-08, 2023 ambapo takribani 6000 wa ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki kwenye mkutano huo.
Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepewa mafunzo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ili kuwawezesha kufanya tathmini stahiki kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini.

Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku tano kuanzia Jumatatu Mei 22, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewataka washiriki kuzingatia elimu watakayoipata.

“Mkahakikishe tathmini zinafanyika kwa usahihi na wafanyakazi watakaopata majanga ya ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wapate fidia stahiki na kwa wakati. Hii itaongeza ari kwa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii wakijua wana uhakika wa kinga ya majanga kazini” amesema Masala.

Masala ambaye amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla ameongeza kuwa ni vyema waajiri wakahakikisha wafanyakazi wao wanajiunga na mfuko wa WCF ili kuondolewa mzigo wa gharama za majanga mbalimbali yanayoweza kutokea kazini.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, amesema mafunzo hayo yatawaongezea weledi madaktari hao kufanya tathmini sahihi na kwa wakati hatua itakayosaidia pia wafanyakazi wanaopata majanga kazini kulipwa fidia stahiki na kwa wakati.

Baadhi ya madaktari walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi wamekiri kuwa yatawaongezea ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi zaidi na hivyo WCF kulipa fidia stahiki.

Mfuko wa WFC ulianza kutoa huduma kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini mwaka 2016 ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa, ukichukua nafasi ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo ilionekana kutotoa fidia stahiki kwa wafanyakazi waliopata majanga kazini.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanaoumia wakiwa kazini.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Mei 22, 2023.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu WCF.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera ili kuwaongezea ujuzi wa kufanya tathmini kwa wafanyakazi wanaoumia kazini (kupata ajali, kuugua ama kufariki wakiwa kazini) ili kupata fidia stahiki na kwa wakati kutoka WCF.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo hayo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi amesema mafunzo hayo ni muhimu na yatawasaidia kufanya tathmini kwa weledi zaidi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini.
Daktari kutoka Hospitali ya Magai Kahama, Dkt. Peter Magai akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo ambao ni pamoja na kuwawezesha madaktari kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa WCF wanaoumia kazini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Madaktari walioshiriki mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.