Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 14, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dodoma. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 14, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma (kushoto) wakionesha begi la fomu za uteuzi.

Wagombea wakielekezwa namna ya kujaza kitabu cha kuchukua fomu
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe akisaini fomu za uteuzi. Mgombea Mwenza, Mhe. Shoka Khamis Juma akisaini kitabu.

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza.



Dodoma, Agosti 14, 2025 – Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, leo amemkabidhi rasmi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Wilson Elias Mulumbe.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika makao makuu ya INEC jijini Dodoma, ambapo Mulumbe aliambatana na mgombea mwenza wake, Mhe. Shoka Khamis Juma. Tukio hilo limeashiria kuanza kwa maandalizi ya kampeni rasmi za chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza mara baada ya kupokea fomu, Mulumbe alisema ADC inalenga kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli kupitia sera za uchumi shirikishi, uwekezaji kwenye elimu, na mageuzi ya mifumo ya afya. "Tunakwenda kuomba ridhaa ya wananchi kwa dhamira safi na maono ya kulibadili taifa letu kuwa la ushindani kimataifa," alisema.

Kwa upande wake, Jaji Mwambegele aliwakumbusha wagombea wote kuheshimu taratibu za uchaguzi na kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni zilizowekwa na Tume. Pia alibainisha kuwa zoezi la uteuzi wa wagombea urais litafanyika Agosti 27, 2025.

Hadi sasa, vyama vimeendelea kuchukua fomu za kugombea nafasi za urais na makamu wa rais, huku hamasa ya kisiasa ikizidi kupanda nchini kote kuelekea siku ya kupiga kura.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: