Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa (kulia) na Mfalme Mswati III wa Eswatini katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na viongozi wengine katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).

Na Mwandishi Wetu.

CAPE TOWN, AFRIKA KUSINI – Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, yupo Cape Town kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika, tukio la kihistoria lililoandaliwa chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika (AU), Jopo la Ngazi ya Juu la Uwekezaji wa Maji Afrika na Urais wa Afrika Kusini katika Kundi la Nchi 20 (G20).

Mkutano huo umeitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).

Jopo hilo lina Wenyeviti Wenza Watatu – Rais wa Namibia, Rais wa Senegal, na Waziri Mkuu wa Uholanzi – huku wajumbe wake wakiwemo Marais wa Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Gambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mfalme wa Morocco.

Dkt. Kikwete anashikilia nafasi ya Mwenyekiti Mwenza Msaidizi (Alternate Co-Chair), akisaidia Wenyeviti Wenza katika utekelezaji wa majukumu ya jopo hilo.

Mwaka huu, Afrika Kusini inashikilia Uenyekiti wa G20, na viongozi wa Afrika wanaokutana Cape Town wameazimia kuhakikisha Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika inapata kipaumbele katika ajenda za mkutano wa G20 unaotarajiwa kufanyika Novemba 2025 mjini Cape Town.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: