Na Mwandishi Wetu.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo tarehe 14 Agosti 2025 imeanza rasmi zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi za Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nafasi za Udiwani kwa Tanzania Bara, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Zoezi hilo litadumu hadi tarehe 27 Agosti 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, R.K. Kalima, amesema wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo yote watakuwa wakitoa fomu hizo kwa wagombea ubunge katika ofisi za wasimamizi hao, huku wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wakitoa fomu za wagombea udiwani.

Wanachama waliopendekezwa na vyama vyao wanatakiwa kufika wakiwa na barua ya utambulisho kutoka chama husika kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:00 alasiri.

Aidha, Tume imewataka wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Katiba, sheria na kanuni katika mchakato mzima wa 

Tume pia imepongeza vyama vya siasa kwa kuendelea na maandalizi, huku ikisisitiza kauli mbiu yake: “Kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura.”

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: