Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Asasi za Kifedha Tanzania (TAMFI) limesema lina programu maalumu ya kuchangia uhifadhi wa mazingira na kupambana na ukataji miti kwa kuwezesha nishati safi ya kupikia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMFI, Winnie Terry katika kongamano la Wanawake katika fedha:Kukumbatia mabadiliko ya tabia nchi lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Alisema katika kongamano hilo lenye nia ya kuchanganya jinsia na uendelevu wa mazingira ndani ya sekta ya fedha, kuwa kuna haja kwa wadau kama wao kuchukua hatua na kuunga mkono juhudi za serikali kukabili mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwezesha wanawake nishati safi ya

"Ahadi yetu ya 'Kukumbatia Mabadiliko ya Tabianchi' inazidi mjadala tu; ni wito wa kuchukua hatua. Kwa kulingana na maono ya serikali ya ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, tunalenga kushughulikia vipengele muhimu vya maji, nishati mbadala, na mabadiliko ya tabianchi na kujitolea kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu namba kumi na nne (14)" alisema Winnie.

Mkutano huo uliopata ufadhili kutoka Foundation ya Charles Stewart Mott uliweka wazi ushawishi muhimu wa taasisi za kifedha kuwezesha wanawake ndani ya sekta ya fedha kuongoza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAMFI, Devotha Ntuke Minzi alisema ni jukumu la wanawake kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

Akisisitiza athari zisizo sawa za mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake, hasa nchini Tanzania na kote duniani, Minzi alitaka ushirikishi katika kufanya maamuzi na kutekeleza mipango kwa vitendo. Alihimiza haja ya kuongeza sauti za wanawake katika fedha kama waendeshaji muhimu wa suluhisho endelevu kwa changamoto hizi za kimataifa.

Naye Ofisa Programu wa TAMFI, Deodati Bernard alielezea mchango mkubwa wa wanawake kwa maendeleo ya Tanzania.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa wanawake na Wakurugenzi Mtendaji kutoka Taasisi za Fedha za Daraja la Kwanza na la Pili, pamoja na wajumbe kutoka Chama cha Benki Tanzania (TBA), Chama cha Nishati Mbadala Tanzania (TAREA), Mtandao wa Maji na Usafi Tanzania (TaWaSanet), New Faces New Voices (NFNV), Amshaamsha Foundation, IMED Foundation, Elico Foundation, Water.org, Kampuni ya Huduma za Nishati Endelevu (SESCOM) na wanawake katika nyanja mbalimbali za mfumo wa mabadiliko ya tabianchi nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: