Wito huo ulitolewa na Meneja wa Elimu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Manoah William wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini Tanga.
Alisema kwamba iwapo watoto wa kike hawatashika elimu ambayo ndio nguzo kuu katika maisha ikiwemo kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao hawawezi kufanikiwa badala yake watajikuta wakirudi nyuma kimaendeleo kila siku.
“Lakini kuweza kupata usawa huo lakini wanatakiwa kupambana hakuna lelemama wapambane wafikie malengo yao hakuna mtu ambaye anaweza kumshika mkono kila siku wapambane washike elimu, wajiamini wajitambue watafanikiwa”Alisema.
Aidha alisema Shirika hilo wameungana na halmashauri ya Jiji la Tanga kusherehehe siku ya mtoto wa kike duniani lengo kubwa wao wanafanya kazi na watoto wa kike kwa mapana wamekuwa wakisaidia wasichana zaidi ya 600 katika mkoa wa Tanga.
“Leo tumeungana na serikali kuchagiza maendeleo ya mtoto wa kike kwenye elimu na ujasiriamali na biashara lengo lao mtoto wa kike lazima aweze kujitambua kupata nafasi sawa kwenye jamii aweze kuinuka aweze kujitegemea mwenyewe”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba wanaiomba Serikali iweze kuunga mkono juhudi hizo waweze kufanya kwa mapana yake kumsaidia mtoto wa kike aweze kujiwezesha mwenyewe katika elimu na brac wanafaya na wanawasaidia watoto wake kike.
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Fatma Kalovyia alisema Serikali ya awamu ya tano dkt Magufuli inaendelea kuunga mkono juhudi za watoto wa kike ili kujenga Taifa kwenye usawa.
Alisema serikali kupitia program mbalimbali za uwezeshwaji umefanikiwa kuweka mazingira wezesha kwa watoto wa kike kujitambua ili waweze kufikia mafanikio ambayo yatawawezesha kiuchumi
“Kauli mbiu ya mwaka huu ni tumuwezeshe mtoto wa kike kujenga Taifa lenye usawa kubadilisha mtazamo na maisha ni la kwako mwenyewe tuwasiwategemee watu wengine kuwabadilisha maisha”Alisema
Hata hivyo alisema mtoto wa kike ana haki ya kusoma kulindwa ikiwemo kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozihata wakiwemo vyuoni na shule za sekondari na msingi ili waweze kujijenga uzoefu hata wanaposimama mbele za watu waweze kujiamini na baadae waweze kuwa viongozi bora.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Mtoto Mwajuma Adamu alitoa wito kwa kwa kuwalinda watoto wa kike kwenye changamoto ambazo wanakutana nazo masualaa ya ukatili, ubaguzi, kukoseshwa haki zao za msingi kama elimu mavazi na kulindwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: