Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akimuombe kura Mgombe Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ametangaza neema kwa wavuvi kwenye Jiji la Tanga baada ya kuwahaidi kwamba watawezeshwa kupata mikopo nafuu na zana za kisasa za uvuvi ili waweze kunufaika kupitia sekta hiyo na hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na hilo amehaidi pia kuipatia ufumbuzi changamoto ya barabara ya kwenda Machinjioni –Msikitini ili kuhakikisha inakuwa kwenye kiwango kizuri kuliko ilivyokuwa sasa.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika Dunia Hotel Kata ya Mzingani Jijini Tanga uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.
Alisema kwamba suala la wavuvi atalishughukia kwa kuhakikisha changamoto ambazo wanakabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao anazipatia ufumbuzi ili kuwawezesha kufanya shughuli hizo bila vikwazo.
Ummy alisema pia atahakiksha anawezesha mazingira ya uwepo wa barabara ya Mzingani hadi Machinjioni kwa kupasua barabara ya mtaa wa msikitini ili kuwawezesha wananchi kuitumia kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali
“Kuhusu suala la taa za barabara nitalifanyia kazi kuhakikisha mitaa yote muhimu kwenye kata ya Mzingani inawaka nyakati za usiku kuweza kulinda usalama wa watoto hivyo ninawaomba wananchi wa Mzingati mnichague kwani nina mipango mingi ya kimaendeleo lakini pia Octoba 28 mchagueni kwa kuwa nyingi za kishindo Rais Dkt John Magufuli“Alisema
Hata hivyo alisema katika kipindi cha Miaka mitano iliyopita Serikali ya CCM ilijielekeza katika kujenga Miundombinu ya Hospitali, Zahanati na Vituo Afya na kuwa katika miaka mitano ijayo CCM itajielekeza ktk kuhakikisha maboresho ya bima ya Afya ili watu wengi waweze kupata huduma za Afya bila vikwazo.
Sambamba na hilo Ummy alieleza kuhusu suala la CT Scan ambapo aliwaambia wana Mzingani kwamba kuna maneno yanaelezwa kwamba alichukua CT Scan Mashine ya Bombo na kuipeleka Hospitali ya Mwananyamala DSM.
“Labda niwaambieni wapuuzeni maana wameanza kupagawa kwanza sisi hatukuwa na hiyo mashine ila kuna mdau alitaka kutusaidia ikabidi tutafute fedha za kujenga Jengo kwa ajili ya kuiweka mashine hiyo ambayo itasaidia sana kupunguza safari za kwenda Kilimanjaro na tayari fedha zimeshapatikana”Amesema Ummy Mwalimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: