Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Domingos Gove akizungumza na wanahabari za mikutano ya SADC inayoendelea jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imesema ipo kwenye mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa kanda kwa ajili ya kusaidia nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa jumuiya hiyo Domingos Gove wakati anazungumza na waandishi wa habari za mikutano y SADC inayoendelea jijini.
“Kwa sasa tupo katika mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ambao lengo ni kuhakikisha tunasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC,” amesema Gove.
Amefafanua katika mkakati huo pia watahakikisha kunakuwa na miundombinu itakayofanikisha nchi wanachama zinajikita kwenye kilimo kwa ajili ya kupata chakula cha kutosha kwa nchi zao.
Ameongeza kuwa kwenye mfuko huo ambao utaanzishwa kwa nchi za SADC utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala la kilimo.
Pia amesema mikakati mingine ni kuongeza ushindani na uzalishaji wa nafaka pamoja na kuhakikisha kunakuwa na sera ya kulinda usalama wa chakula.
“Tumejipanga kuhakikisha kupitia mfuko huo wa kilimo tunazalisha chakula kwa wingi na pale ambapo nchi mojawapo itakuwa na tatizo la uhaba wa chakula basi tunasaidia kupeleka chakula kutoka kwenye nchi zenye chakula cha ziada,”amesema.
Ameongeza vyakula ambavyo vitazalishwa pamoja na mambo mengine vitazingatia suala la lishe kuhakikisha walaji wanakuwa na afya njema na imara kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo kwa nchi wanachama.
Wakati huo huo jumuiya hiyo imeeleza namna ambavyo imejipanga katika kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinakuwa na miundombinu yenye uhakika.
Ambapo kwenye eneo hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Habari, Matangazo na Machapisho ya Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya SADC Zamarad Kawawa ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyoweka mkazi katika ujenzi wa miundombinu.
“Tanzania tuko vizuri, katika eneo hilo, ukienda bandarini, viwanja vya ndege, reli, na barabara kote kumeimarika kwa kiwango kikubwa,” amesema Kawawa ambaye pia nia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
Toa Maoni Yako:
0 comments: