QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ambayo ni mshirika rasmi wa Timu ya mpira wa miguu ya Manchester City, Ikiwa kama sehemu ya ahadi yake ya kuendeleza vipaji na kama namna ya kampuni kurudisha kwa jamii, imedhamini wachezaji watatu chipukizi wa kiafrika kuhudhuria mafunzo ya mpira wa miguu ya jijini Manchester (City Football Language School in Manchester).

Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ya Manchester ni kozi ya wiki mbili ya mpira wa miguu na mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wachezaji chipukizi (vijana). Kozi hii ilianza tarehe 28 Julai na itakamilika tarehe 12 August mwaka 2019.

Wachezaji hao chipukizi walichaguliwa kutoka katika mchakato wenye ushindani mkubwa nchini Ghana, Cameroun na Ivory Coast, na ni kozi ambayo haina gharama yoyote kwa wachezaji hawa walio chaguliwa.

Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ni kozi ya lugha ya kiingereza na mpira wa miguu yenye hamasha kwa wachezaji chipukizi wenye umri wa kati ya miaka 12-17, ambayo inafanyika katika viwanja vya mafunzo vilivyoko huko katika jiji la Manchester. 

 Wachezaji chipukizi waliochaguliwa wanapata fursa ya kupata falsafa ya mafunzo na mbinu za mpira wa miguu za manchester city kupitia katika vipindi vya mafunzo ambavyo vinaongozwa na makocha wa mpira wa miguu wa jiji la manchester. 

 Vile vile wanapata fursa ya kuendeleza uwezo na ujuzi wao wa kutumia lugha ya kiingereza kupitia majadiliano katika vipindi vya ulimwengu wa mpira (the world of football) kutoka kwa walimu wa vituo vya mafunzo ya lugha vya British Study Centres.

Wachezaji hao chipukizi wanajifunza na kupata mafunzo nyumbani au katika makao makuu ya machester city katika kitovu cha campus ya Etihad, sehemu ambayo watakuwa na nafasi ya kutumia miundombinu bora.
Mafunzo ya Mpira wa miguu yenye ubunifu wa kiwango cha juu na Mtaala wa Lugha ya Kiingereza vimeandaliwa kwa lengo la kuhakikisha wanaongeza uwezo wa kujifunza nje na ndani ya uwanja, ikiwa inagusa maeneo ya msingi ya maisha ya mtaalamu wa mpira wa miguu. Zaidi ya kutambuliwa na Shule ya Lugha ya kiingereza ya British Council, kozi hii vile vile inatambuliwa na Eaquals ambao lengo lao ni kuthibitisha kwamba viwango vya juu katika kufundisha lugha na mafunzo vinafikiwa duniani kote.

Akiongelea kuhusu fursa hiyo, Bwana Biram Fall; Meneja Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara alisema: "QNET inaendelea kuwekeza katika kuendeleza na kukuza vipaji katika ngazi zote. Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja ni moja kati ya majukumu yetu katika mpira wa miguu na ari ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. 

Mchezo wa mpira wa miguu unaunganisha watu kutoka katika asili na maeneo mbalimbali. Mpira wa miguu vile vile unahamasisha kufanya kazi kwa pamoja kama timu, kuwa na ari ya timu, kufanya kazi kwa nguvu na hamasa. Hizi ni baadhi ya tunu za msingi za QNET kama biashara."

Katika Afrika, QNET ni mshirika wa mauzo ya moja kwa moja Ligi ya mabingwa CAF, Kombe la Shirikisho la Total CAF na Kombe la Total CAF Supa Cup (Total CAF Champions League, Total CAF Confederation Cup and the Total CAF Super Cup).

QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali katika bara la Afrika, huku ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. 

Katika mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtandao kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: