Akizungumzia hali za wagonjwa wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Dkt. Elisha Esati amesema wagonjwa waliohamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ni wameungua Zaidi ya asilimia 80 mpaka 90 na wengi wao ni vijana.

Helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, ikitua viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo Agosti 11, 2019 ikileta majeruhi wane wa ajali ya moto uliosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta mkoani Morogoro Jumamosi Agosti 10, 2019.
Wafanyakazi wa afya, wakimshusha majeruhi kutoka kwenye helikopta hiyo.
Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw., Aminieli Eligaesha, akizungumza na simu katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam kuisubiri helikopta ya JWTZ iliyoleta majeruhi wane wa ajalki ya moto.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga (kushoto), akiwapa maelekezo wahudumu wa afya wanaosubiri helikopta kutua viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam Agosti 11, 2019.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga (kulia) na Msemaji wa Hospitali hiyo, Bw. Aminieli Eligaesha, wakijadiliana jambo eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dar es Salaam.

HELIKOPTA ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imewasafirisha majeruhi wanne wa ajali ya moto leo Agosti 11, 2019 kutoka Morogoro kuja Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Majeruhi hao ni wale walionusurika kutokana na moto uliozuka baada ya lori la mafuta kupinduka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro Agosti 10, 2019 na baadaye watu kuelekea eneo hilo kuchota mafuta kabla ya kutokea moto mkubwa na kuunguza watu na mali zilizokuwa katika eneo hilo.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminieli Eligaesha amesema, majeruhi hao wanafanya idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali hiyo kutokana na tukio hilo la kusikitisha kufikia 46, watatu kati yao tayari wamefariki dunia.

Taarifa zinasema idadi ya watu waliofariki kutokana na tukio hilo imefikia 69 sasa, kwa mujibu wa Televisheni ya Taifa TBC huku majeruhi wakifikia 67.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: