NA ALLAWI KABOYO - MULEBA.


Mwenyekiti mtendaji wa taasisi ya Tanzania Charitable and Development Oganazation (TCDO) inayojishugurisha na kusajili, kuhamasishana kuwasafirisha waislamu kwenda kufanya ibaada ya Hijja, amenusurika kichapo kutoka kwa waumini wa dini hiyo.

Mwenyekiti huyo anayefahamika kwa jina la SUEDI TWAIBU SUEDI alikutana na dhahama hiyo April 2, 2019 katika msikiti wa Nuru uliopo wilayani Muleba Mkoani Kagera alipofika akiwa mingoni mwa taasisi 12 zinazohamasisha waislamu kujitokeza kwenda kufanya ibaada ya Hijja ambayo ufanyika nchini Saudiarabia kila mwaka.

Hali hiyo ilitokea baada ya mmoja wa mumini waliokuwepo msikitini hapo kumuuliza swali kiongozi wa msafara huo aliyejitamburisha kwa jina la Mussa Yusuph Kundecha lililomuhitaji kuwaeleza waislamu kuwa ni vigezo gani vilitumika kuisajili upya taasisi ya TCDO kwa kuwa mwaka 2017 taasisi hiyo iliwatapeli baadhi ya waislamu waliojiandikisha kwaajili ya kwenda Makka kufanya ibaada ya Hijja na hadidi sasa waumini hao hawajarudishiwa fedha zao?

Swali hilo liliibua mjadala mzito na kusababisha kuwepo kwa viashiria vya kuvunjika amani baada ya kiongozi huyo kujibu kuwa atalipeka suala hilo katika ofisi ya Mufti kutokana na kuwa nje ya uwezo wake.

Hata hivyo waumini hao hawakuridhika na majibu hayo na kumtaka mtuhumiwa kujibu mwenyewe tuhuma zinazomkabili ambapo aliwaomba radhi waumini hao pamoja na viongozi aliokuja nao na kusema kuwa,

“Ni kweli nakili kutokea kwa tatizo hili lililosababishwa na taasisi yangu na kuwafanya waislamu wengi kutafanya ibaada hii mnamo mwaka 2017 akiwemo mzee Shaban Khamis, tatizo hili halikutokea kwenye taasisi yangu pekee bali lilitokea kwenye baadhi ya taasisi nyingine lililosababishwa na mtandao kuruka.”

Bwana Suedi aliongeza kuwa hakuwahi kupata nafasi ya kuwaeleza waislamu juu ya tatizo lililotokea na kuongeza kuwa taasisi yake inauzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 18 na hakuwahi kukutana na tatizo hilo suala lilosababisha kuwepo kwa kurushiana maneno ya hapa na pale ambapo walimtaka kurejesha fedha za waislamu waliotapeliwa.

Akiongea kwa masikitiko makubwa mmoja wa wale waliotapeliwa na kushindwa kufanya ibaada ya Hijja ambapo ameeleza alivyoachwa uwanja wa ndege huku akiwa tayari alikuwa ameshalipia kila alichohitaji kulipia kwaajili ya safari.

“Ilikuwa tarehe 18 mwezi wa 8 mwaka 2017 ambapo waumini tulitakiwa kufanya safari ya kwenda Hijja na nilikuwa nimelipa kiasi cha shilingi milioni 9.7 katikia taasisi ya TCDO ambayo mwenyekiti wake ni Suedi Twaibu Suedi na fedha hiyo ilitosha kukagaramia safari ya kwenda na kurudi pamoja na maradhi na chakula.” Alisema mzee Shabani.

“Tarehe hizo hatukuondoka tulianza kupewa semina ya Hijja na kuambiwa tutaondoka tarehe 22 mwezi wa 8 mwaka 2017 hivyo tulijiandaa na siku ilipowadia nilienda uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam nikiwa na jamaa zangu kutoka Tanga na wao walikuwa wakisafiri, kilichotushangaza hatukuwa na msindikizaji ambaye alitakiwa kutupeleka bwana Suedi, tulikaguliwa mizigo yetu tukawaaga jamaa zetu tulivyoingia ndani kwenye chumba cha abilia Yule jamaa anayekagua tiketi alitwambia tiketi zetu ni feki hivyo tunatakiwa kutoka mahali pale.” Mzee Shabani alieleza.

Mzee Shabani alisema kuwa baada ya kufukuzwa uwanja wa ndege walianza kumtafuta mwenyeji wao bila mafanikio kwa kuwa simu zake zilikuwa hazipokelewi na kuamua kuchukua hatua za kisheria ambapo kilio chake kikubwa ni kurudishiwa fedha zake.

Aidha Waumini wa dini ya Kiislamu nchini wamehamasishwa kujiandaa na ibaada ya hijja kutokana na utaratibu kubadirika ambapo wale wote wanaohitaji kufanya ibaada hiyo tukufu wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao kabla ya tarehe 30 SHAABAN.

Kufuatia kuwasili kwa taasisi hizo wilayani Muleba, Sheikh wa wilaya hiyo Sheikhe Zakharia pamoja na imaamu mkuu wa wilaya hiyo Ust.Idd Suedi waliwatahadharisha waislamu kuhusu taasisi zisizo na uaminifu zinazoweza kuwapelekea kutapeliwa na kushindwa kufanya ibaada takatifu ya Hijja na kuiomba serikali kuzichukulia hatua taasisi zinazowatapeli waislamu fedha zao ikiwemo kuzifutia usajili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: