Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile akieleza Jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu majadala wa Wadau wa habari na Serikali, Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utetezi kutoka Jukwaa la Wahariri la Kimataifa, IPI, Ravi R. Prasad, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri la Kimataifa, IPI, Khadija Patel, kushoto ni Naibu Mkurugenzi , IPI, Scott Griffen na Mkuu wa Akademi, DW, Carsten von Nahmen.
Naibu Mkurugenzi , IPI, Scott Griffen, akiongea jambo kwa Waandishi wa Habari( hawapo pichani) kuhusu kufurahishwa kwake na Serikali ya Tanzania kuitikia wito wa wadau wa habari, katika mkuatno uliofanyika Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile na Mkuu wa Akademi, DW, Carsten von Nahmen.

Waandishi wa Habari wa Kimataifa wamefurahishwa na Mwitikio wa Serikali kwa itikio la kukaa na wadau wa sekta ya Habari kwa lengo la kuboresha utendaji wa sekta hiyo nchini .

Wakizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Kimataifa, IPI, Khadija Patel ameelezea hatua walizofikia baada ya kukutana na viongozi mbalimbali, jambo ambalo limewaridhisha waandishi hao na hivyo kuipongeza Serikali kwa hatua hizo za wali, na kusema maafikiano yataboresha utendaji wa kazi katika sekta ya Habari.

“Sisi kama Taasisi ya Habari ya Kimataifa (IPI), tumefurahishwa na Serikali kukubali kufanya majadiliano, kuboresha ubora wa vyombo vya Habari, tumekutana na Waziri wa Habari, tunashukuru alitusikiliza na tumefurahishwa kwa kukubali kwake kuboresha uelewa baina ya Serikali na Wadau wa sekta ya Habari nchini”, Khadija Patel, Makamu Mwenyekiti, IPI alisema.

Naye Mkuu wa akademi ya chombo cha Habari (DW) kutoka Ujerumani ambaye pia ni Mwandhishi mkongwe wa chombo hicho, Carsten von Nahman, alieleza furaha yake kwa Serikali ya Tanzania kufungua mlango wa mjadala kuhusu uboreshaji wa vyombo vya Habari, na amesema kuwa hatua hiyo ni bora zaidi kwani itawasidia Waandishi pia kuboresha utendaji na kuacha kulalamikiwa na Watendaji wa Serikali.

“tumefurahishwa na mwitikio wa Serikali kuungana na wadau wa sekta ya Habari katika kubadilishana mawazo kwa kuangalia mbele zaidi katika kuijenga sekta hii, lakini katika mikutano tuliofanya na viongozi wa Serikali, kuna madai ya ubora na maadili kwa Waandishi kutozingatiwa kwa hiyo hatua hii ya mjadala itaboresha utendaji kwa Waandishi wa Habari”, Carsten von Nahman, Mkuu wa akademi, DW.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi, , IPI, Scott Griffen, yeye aliweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania imeonyesha nia ya kufanya mazungumzo kwa nia ya kuboresha sekta hiyo na amesema kuwa ni muda mzuri wa vyombo vya Habari kujiweka katika nafasi nzuri ya utendaji kazi.

“Serikali ina Mtazamo wa wazi katika suala hili lakini pia kwenye mazungmzo haya wadau pamoja na wamiliki wa vyombo vya Habari ni muda mzuri kuwa katika haya mazungmzo ili kuweka sekta ya Habari katika utendaji mzuri”, Scott Griffen, Naibu Mkurugenzi , IPI alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, Deodatus Balile amewaasa wanahabari kutekeleza kazi kwa ubora na maadili makubwa ili kuonyesha weledi katika tasnia hiyo.

“kuna malalamiko kwa upande wa viongozi wa Serikali kuwa kuna upungufu wa kiwango cha weledi kwa sisi waandishi wa Habari, kwamba kiko chini kidogo, kwa hiyo wanapenda kuona na sisi utendaji wetu kazi tunauboresha kidogo”, alifafanua Bw. Deodatus Balile.

Aidha Mwenyekiti huyo wa TEF amewataka Waandishi kuwa na weledi ili siku moja Tanzania iwe na vyombo vya Habari ambavyo vikifanya kazi havilalamikiwi wala vyenyewe havilalamiki, na alisema kuwa IPI iko tayari kuwasaidia wanahabari katika kuongeza kiwango cha elimu katika mafunzo mbalimbali na kubadilishana uzoefu ndani na nje ya nchi.

Balile alisema kuwa ugeni huo ambao umeshirikisha watu sita kutoka Jukwaa la Wahariri la Kimataifa,IPI umekutana na viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassimu Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, na wamefurahishwa na mwitikio wao katika suala hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: