Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya maafisa ughani yaliyoandaliwa na Serikali ya watu wa China kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo cha China kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne SUA, ufunguzi huo ulifanyika Julai 10 mwaka huu katika chuo kikuu cha SUA.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka china watakaoendesha semina ya mafunzo kwa Maafisa Ughani yanayo husu kilimo chenye tija. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo Dkt.Marry Mwanjelwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa mabalimbali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo Dkt.Mary Mwanjelwa na kulia kwake ni Afisa kutoka Ubalozi wa China Prf. Lin Zhiyong.
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt.Mary Mwanjelwa wakati akitoa hotuba yake mbele ya wandishi wa habari na kukazia Maafisa ughani kutokaa maofisini.
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt.Mary Mwanjelwa akiwasili kwenye viwanja vya SUA ulipofanyika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa Maafisa Ughani wa Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dodoma. Kulia ni Prof. Peter Gilla aliyemuwakilisha Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne.
Prf. Li Xiaoyun kutoka Kitivo cha masuala ya kilimo katika Chuo kikuu nchini china
Prf. Lin Zhiyong, Afisa kutoka Ubalozi wa China.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amewataka wananachi wa Mkoa wa Morogoro kuachana na kilimo cha mazoea badala yake kujielekeza kwenye kilimo chenye tija ili kupata mazao mengi kwa gharama ndogo yatakayowasaidia kujikwamua na umasikini.
Dkt. Kebwe ameyasema hayo Julai 10 mwaka huu wakati akizindua mafunzo ya kilimo kwa maafisa ughani kutoka Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dodoma yatakayofanyika kwa wiki mbili katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne ( SUA) kuanzia Julai 10 mwaka huu.
Dkt. Kebwe aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo amewataka Maafisa ughani wanaoshiriki mafunzo hayo yanayotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo cha nchini humo (CAU) ambapo amewataka baada ya kupata elimu hiyo utekelezaji wake uanze mara moja kwa kuwafundisha wananchi kulima kilimo cha Biashara na sio kilimo cha mazoea.
Aidha, Dkt. Kebwe ametumia fursa hiyo kuihakikishia nchi ya china utajiri wa Mkoa wa Morogoro, usalama, amani na hali nzuri ya hewa hivyo kupitia mwakilishi wa Ubalozi wa China Bw. Lin Zhiyong ameomba kuwashawiwshi wawekezaji nchini mwake kuja kuwekeza Viwanda Mkoani Morogoro.
Akiongea muda Mfupi kabla ya Mgeni Rasmi kutoa hotuba yake, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa ameendelea kutoa maagizo kwa wataalamu wa Kilimo hususan Maafisa ughani kutokaa Ofsini na kwamba ofisi zao ziko mashambani, huko wawaelimishi wakulima, kujihusisha na kilimo chenye tija.
Hata hivyo, Dkt. Mary amebainisha kuwa viwanda vinategemea mali ghafi inayotokana na Kilimo hivyo, amesema tunapozungumzia viwanda tunazungumzia kilimo kwa kuwa asilimia 80 ya mali ghafi ya viwanda inatoka shambani na kubainisha kuwa kilimo ni sekta wezeshi ya viwanda hivyo hakuna budi kujikita hasa kwenye kilimo chenye tija.
Imeelezwa kuwa elimu ya kilimo hicho chenye tija inayotolewa marafiki zetu kutoka China kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA pamoja na Sekretarieti ya Mkoa kimekwisha nufaisha wakulima wengi hasa wa vijiji vya Mtego wa samba kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Kijiji cha Peapea kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: