Na Mwandishi Wetu.

Serikali kupitia Wizara ya Afya Tanzania imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ongezeko la magonjwa ya mlipuko ikiwemo mafua makali ya Influenza, UVIKO-19, homa ya Dengue na Kipindupindu, huku ikisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za kinga ili kulinda afya za jamii.

Taarifa hiyo iliyotolewa Dodoma Februari 25, 2026 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace E. Magembe, imeeleza kuwa magonjwa ya njia ya hewa huongezeka zaidi katika kipindi cha miezi ya Novemba hadi Aprili, hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia usafi binafsi, kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

Aidha, Wizara imeonya kuhusu hatari ya homa ya Dengue inayosambazwa na mbu aina ya Aedes, hasa katika maeneo yenye maji yaliyotuama. Wananchi wametakiwa kuharibu mazalia ya mbu kwa kufukia madimbwi, kuondoa vyombo vinavyoweza kuhifadhi maji na kutumia kinga dhidi ya mbu.

Kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu, serikali imesema nchi imepiga hatua katika kudhibiti mlipuko huo, lakini bado ipo hatarini kutokana na mvua zinazoendelea na uwepo wa maambukizi katika nchi jirani. Wananchi wametakiwa kuchemsha au kutibu maji ya kunywa, kuzingatia usafi wa chakula na mazingira, pamoja na kuwahi vituo vya afya wanapopata dalili.

Serikali imewahakikishia wananchi kuwa itaendelea kufuatilia mwenendo wa magonjwa hayo na kutoa taarifa zaidi kadri itakavyohitajika, huku ikisisitiza ushirikiano wa jamii katika kuchukua tahadhari ili kuzuia maambukizi.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: