Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Hassan Kisabya Almas. Mgombea huyo wa NRA aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Hamisi Ally Hassan (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).
Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Hassan Kisabya Almas (kulia) akiwa na Mgombea mwenza, Mhe. Hamisi Ally Hassan (kushoto) wakionesha mkoba ulio na fomu za uteuzi wa nafasi hizo waliokabidhiwa na Tume leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima, akizungumza.

Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Hassan Kisabya Almas akisaini kitabu.




Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhan Kailima, akizungumza.
DODOMA – Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, leo Agosti 9, 2025, amemkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Hassan Kisabya Almas.

Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Tume, Njedengwa jijini Dodoma, yalishuhudiwa na viongozi wa NRA na watendaji wa INEC. Mgombea huyo aliambatana na mgombea mwenza wake, Mhe. Hamisi Ally Hassan, pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu, Mhe. Kisabya aliahidi kuendesha kampeni zenye kuzingatia maadili ya uchaguzi na kuwaletea Watanzania sera mbadala za kuharakisha maendeleo ya taifa.

Asubuhi hiyo katika mwendelezo wa zoezi la uchukuaji fomu, Mgombea wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongozana na mgombea mwenza wake Dkt. Emmanuel Nchimbi, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuchukua fomu hizo za kuwania nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa chama na serikali.

Ratiba ya Uchukuaji Fomu za Uteuzi wa Wagombea wa Urais na Makamu wa Rais:

Tarehe 9–14 Agosti 2025: Wagombea kuchukua fomu katika Ofisi za INEC, Njedengwa – Dodoma.

Tarehe 15–25 Agosti 2025: Kurudisha fomu zilizojazwa kwa ukaguzi wa awali.

Tarehe 27 Agosti 2025: Uteuzi rasmi wa wagombea utakaofanywa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: