
Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Begi lenye Fomu zake za kugombea nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti,
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
DODOMA – Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana amekabidhiwa rasmi fomu za kugombea nafasi hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele.
Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Tume, Njedengwa jijini Dodoma, tarehe 9 Agosti 2025, na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wafuasi wa CCM.
Mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Dkt. Samia aliungana na mgombea mwenza wake, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kuonesha begi maalum lenye nyaraka za uteuzi, ishara ya kuanza rasmi safari ya kuwania urais kwa muhula mwingine.















Toa Maoni Yako:
0 comments: