Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele. Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima akizungumza.
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele
Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala (kushoto)
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele akielekezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg Ramadhani Kailima namna ya kujaza kitabu.
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza, Mhe. Masoud Ali Abdala akisaini kitabu.
Wajumbe wa Tume pamoja na Menejimenti wakiwa katika zoezi la utoaji fomu.
Wanachama wa CCK wakiwa katika utoaji fomu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza.


Toa Maoni Yako:
0 comments: