Wafanyakazi wa kampuni ya Barrick nchini kwa mara nyingine wameshiriki mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kujumuisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo makampuni makubwa ya hapa
Kwa kusaidiwa na programu ya kampuni ya Barrick ya kuwataka Wafanyakazi kufanya mazoezi ya kujenga afya washiriki walimudu kukimbia mbio za masafa mbalimbali na baadhi walimudu kukimbia mbio za masafa marefu.
Wakieleza siri ya mafanikio ya kuwa fit kupitia kauli mbiu yao ya ‘We run for fun and healthy’ baadhi ya Wafanyakazi walipohojiwa walisema Barrick inayo sera madhubuti katika kusaidia wafanyakazi kwenye upande wa michezo kwa kuwa na miundombinu ya mazoezi kama gym, swimming pool na viwanja vya mpira wa miguu, kikapu na pete kwenye maeneo ya migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara vilevile Imekuwa ikiwawezesha wafanyakazi wake gharama za kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Kampuni pia kupitia kitengo cha Afya na Usalama huwa inaandaa mashindano ya ndani kwa kushindanisha idara mbalimbali na kualika timu mbalimbali kwa ajili ya kushindana kirafiki ikiwa ni njia mojawapo ya kuweka vizuri afya za mwili na akili za wafanyakazi wawapo kazini.
Barrick pia imekuwa ikiandaa mashindano ya riadha yajulikanayo kama Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka yakihusisha wafanyakazi wake na wadau mbalimbali.
Programu ya uhamasishaji Wafanyakazi kutenga muda hata nusu saa kwa siku kufanya mazoezi ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kuwa mazoezi yanasaidia kuimarisha afya ya akili na mwili. Pia mazoezi yanasaidia kuweza kujikinga na magonjwa nyemelezi yasioambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na unene wa kupindukia.
Wafanyakazi walioshiriki mbio hizi pia walieleza kuwa kupitia michezo mbalimbali wanayoshiriki wanatangaza shughuli za kampuni sambamba na kudumisha uhusiano na wafanyakazi wa taasisi nyingine na jamii kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments: