Matokeo mazuri ya kila jambo yanahitaji maandalizi timamu na ndivyo tunavyofanya kielekea msimu mpya wa ligi daraja la kwanza.

Wakati maandalizi yakiwa yamenoga leo tumetangaza tarehe rasmi ya utambulisho wa timu kwa wakazi wa Temeke na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

Mtendaji mkuu wa klabu Abubakar Jafo (pichani) amewaambia wanahabari kwamba kuanzia leo ni wiki ya REHA FC ambapo kilele chake itakua siku ya jumapili kwenye uwanja wa Bandari Tandika. "Wiki ya Reha itahusisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufungua matawi yetu na kuhitimishwa kwa michezo maalum itakayohusisha timu nne ambazo ni Mtibwa, KMC na Transit Camp na wenyeji Reha fFC" amesema Jafo.

Jafo amesema michezo hiyo itaanza jumamosi kwa mchezo wa mapema saa 8 mchana kati ya Reha dhidi ya Transit Camp na saa 10 jioni Mtibwa itacheza na KMC kisha washindi watacheza fainal siku ya jumapili jioni huku waliofungwa wakicheza mchana. "Siku hiyo tutaitumia kuwatambulisha wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: