MKuu wa Mkoa Dodoma Dr. Binilith Satano Mahenge akihutubia wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru Kwa Mkoa wa Singida, makabidhiano hayo yamefanyika kwenye kijiji cha lusilile ambacho kipo mpakani mwa Dodoma na Singida.
---
Mwenge wa Uhuru leo Agosti 7, 2018 umemaliza mbio zake kwenye jijini Dodoma na kukabidhiwa Kwa Mkoa wa Singida ambapo katika Jijini Dodoma Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa umbali wa KM 1234.5 kwenye Halmashauri zote 8 na kupitia miradi 47 yenye jumla ya thamani Tsh. 23,548,992,580.78. Miradi hii imetekelezwa/inatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali Kuu, Halmashauri ya jiji la Dodoma, Wafadhili wa maendeleo na Wananchi/binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge amesema kuwa Miradi hii ni sehemu tu ya Miradi Mingi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi, ambapo ikikamilika itawanufaisha Wananchi wengi kwenye maeneo husika na watanzania Kwa ujumla.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kwa mwaka huu Mhandisi Charles Francis Kabeho amepongeza Mkoa wa Dodoma na kusema Kuwa miradi Mingi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ipo kwenye Hali Nzuri ya kuridhisha na anategemea kukuta miradi yenye viwango bora kwenye mikoa ambayo inasubiri kukimbiza Mwenge.
Toa Maoni Yako:
0 comments: