Mtendaji Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa, akiongea wakati wa uzinduzi huo
Mtendaji Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa,akiongea na vyombo vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi huo
8.Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo

*Yazindua kampeni ya “Tunaliamsha Kivingine”.

Kutokana na kuimarisha miundombinu ya mtandao wake wa data kwa teknolojia za kisasa zaidi,Zantel inawahakikishia wateja wake kuwa hivi sasa imekuja na nguvu mpya itakayowezesha kupata huduma bora,na huduma za interneti yenye kasi kubwa, gharama nafuu na leo inazindua kampeni mpya kwa wateja inayojulikana kama “Tunaliamsha Kivingine”.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita,Wataalamu wahandisi wa mtandao wa kampuni ya Zantel wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana, wa kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya data,kuhakikisha wateja wanafurahia huduma hiyo kwa kiwango cha juu. Katika kufanikisha kazi hiyo kampuni imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani zipatazo milioni 4.3.

Katika kusherekea ufanikishaji uwepo mtandao bora,Zantel imewaletea watumiaji wa huduma zake waliopo, Zanzibar, Pemba, Unguja na Tanzania Bara kifurushi maalumu cha data cha kuwawezesha kufurahia mashindano ya kombe la Dunia,kupitia promosheni ya “Tunaliamsha Kivingine”.

Akiongea mjini Zanzibar wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu,Mtendaji Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa alisema “Kumekuwa kukitokea mabadiliko ya kila aina katika sekta ya mawasiliano siku hadi siku, ambayo yanatulazimu kwenda nayo sambamba ili kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kupata huduma bora.Kazi tuliyofanya ya kuboresha miundombinu ya mtandao wetu, nawahakikishia wateja wetu wote kuwa huduma za data za Zantel ni bora zaidi kwa sasa na zinawezesha internet yenye kasi kubwa ambayo haijawahi kutokea huko nyuma”.

Aliongeza kusema kuwa kampeni hii imelenga zaidi upande wa Tanzania Visiwani na mikoa ya mwamboa ya Tanzania Bara “Napenda kuwahakikishia wateja wetu wote nchini Tanzania kwamba Zantel tumejipanga kuwekeza zaidi katika kuimarisha miundombinu ya mtandao wetu ili kuhakikisha unakuwa bora zaidi na kuwezesha wateja wetu kufurahia huduma za maongezi ,data na internetI”alisema, Khamis Mussa.

Kampeni ya “Tunaliamsha Kivingine” inakwenda sambamba na kuanzishwa kwa kifurushi kipya cha data kutoka Zantel,kinachowezesha wateja wake kujiunga nacho na kufurahia kuangalia michezo kupitia simu zao na vifaa vyao vingine vya mawasiliano kwa gharama nafuu.

Kifurushi cha Zantel cha Kombe la Dunia kinaanzia shilingi 1,000/-kwa siku,kifurushi cha shilingi 9,000/-kwa wiki na kifurushi cha shilingi 20,000/-kwa mwezi.Vifurushi hivyo vyote 3 vinawezesha kupata data ya 1GB,6GB na 16GB.Vifurushi vya Kombe la Dunia vya data vinapatikana kuanzia vya matumizi ya siku,wiki na mwezi,vinawezesha kuona michezo ya kombe la Dunia kwa programu ya StarTimes tu na kujiunga navyo ni kupitia huduma ya Ezypesa, pekee.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: