Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akiwa ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilinith Mahenge (kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof Faustin Kamuzora (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dk Leonard Maboko (kulia) wakijadili jambo wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu. Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa pili kulia) akipokea maelezo kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa kwanza kulia) akikagua mabanda ambayo yatatumiwa na wananchi kupima VVU katika Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu. Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Mhe Mhagama alikuwa ameandamana na kamati ya maadalizi wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilinith Mahenge, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof Faustin Kamuzora pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dk Leonard Maboko.
---
MAELEZO YA KAMPENI YA KITAIFA YA KUPIMA VVU NA 

KUANZA ARV MAPEMA 

“FURAHA YANGU – PIMA, JITAMBUE, ISHI”

Utangulizi.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI kwa kushirikiana na FHI360 mradi wa USAID –Tulonge Afya na wadau wengine inatarajia kufanya kampeni ya Kitaifa ya Upimaji wa VVU na Kuanza Kutumia ARV Mapema. Kampeni hii inasimamiwa na kikosi kazi kilichoundwa kwa kujumuisha wataalamu toka Wizara yetu, TACAIDS, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na wadau wa VVU na UKIMWI. Jukumu kuu la kikosi kazi ni kusimamia maandalizi, utekelezaji na tathimini ya kampeni ikiwemo kupitia matangazo na machapisho mbalimbali. Kamati hii inaongozwa na wenyeviti ambao NACP na TACAIDS, wakishirikiana na wawakilishi wa TAMISEMI, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kazi za kuweka kumbukumbu zimeongozwa FHI360 Kupitia mradi wa USAID Tulonge Afya.

Hali hali halisi ya maambukizi nchini.

Utafiti wa nne uliofanyika katika ngazi ya kaya kuanzia mwezi Oktoba 2016 hadi Agosti 2017 ulibainisha kuwa wastani wa kitaifa wa maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 ni asilimia 4.7. Wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.1.

Nchi yetu imeridhia na kuanza utekelezaji wa kauli mbiu ya kidunia ya TISINI TATU ifikapo 2020 (asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wawe wamejua hali zao za maambukizo; asilimia 90 ya waliopimwa VVU na kugundulika kuwa wana maambukizo wapatiwe dawa za kufubaza makali ya VVU; na asilimia 90 ya watu wanaotumia dawa wawe wamefubaza VVU). Hali halisi ya utekelezaji wa kufikia hizi tisini tatu ni Kama ifuatavyo:

Tisini ya Kwanza: Nchini Tanzania ni asilimia 52.2 tu ya wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 walitoa taarifa kuwa wanajua hali zao za maambukizo ya VVU (Wanawake ni asilimia 55.9 na Wanaume ni asilimia 45.3)

Tisini ya Pili: Kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ambao wanajua hali zao za maambukizo, asilimia 90.9 walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU (Wanawake ni asilimia 92.9 na Wanaume ni asilimia 86.1)

Tisini ya Tatu: Kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ambao wametoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU, asilimia 87.7 ya watu hao inaonyesha kiasi cha VVU kimefubazwa (Wanawake ni asilimia 89.2 na Wanaume ni asilimia 84)

Hivyo basi, Tanzania inafanya vizuri sana katika Tisini ya pili na tatu, lakini tatizo kubwa ni katika kufikia 90 ya kwanza, kwani ni asilimia 52.2 tu ya wenye VVU wanajua hali zao. Tatizo hili ni kubwa zaidi miongoni mwa wanaume, kwani ni asilimia 45.3 tu ya wanaume wanaoishi na VVU wanajua hali zao.

Jina la Kampeni
Kampeni hii inaitwa “Furaha Yangu” na itafuatiwa na kauli mbiu “tagline” Pima, Jitambua, Ishi Jina na kauli mbiu vimejaribiwa kwa wataalamu na walengwa na kuchaguliwa kati ya majina na kauli mbiu tatu zilizopendekezwa toka kauli mbiu tano na majina matano ya awali.

Madhumuni ya Kampeni.

Madhumini ya kampeni hii ni kufikia malengo ya Tanzania kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 kati yao wanatumia ARV na asilimia 90 ya wanaotumia ARV kiwango chao cha VVU mwilini kinashuka.

Malengo.

Malengo ya kampeni ni kusaidia kutimiza malengo ya Tisini tatu (90 90 90) kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa Kitaifa na Mikoa. Hasa katika mikoa ya utekelezaji wa mradi wa Tulonge Afya (Upande wa Uhamasishaji) na Boresha Afya (Upande wa Utoaji wa Huduma) ambayo ni Arusha, Kagera, Geita, Shinyanga, Kigoma, Mara, Mwanza, Tabora, Singida, Iringa, Njombe, Mtwara, Morogoro, Lindi, Ruvuma, Dodoma Kilimanjaro, Manyara na Simiyu.

Walengwa wa Kampeni

Walengwa wa kampeni hii ni kama wafuatavyo:

Walengwa wa Msingi / Kwanza

Watu ambao hawajawahi kupima VVU na wako katika Hatari ya kumbukizwa au kuambukiza VVU:

Wanaume wenye Umri chini ya Miaka 45

Wasichana walio katika umri wa balehe

Wanawake wenye umri wa miaka 15-24

Akinamama wajawazito

Watu ambao wameambukizwa VVU na hawajaanza kutumia ARV

Akina Mama wanaoishi na VVU na Wananyonyesha pamoja na watoto wao

Walengwa wa Pili

Familia na wale wanaomsaidia mlengwa wa kwanza ikijumuisha watu wenye ushawishi katika jamii na viongozi serikari na viongozi wa dini

Watoa huduma za afya ngazi ya kituo na jamii
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: