Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ashiriki maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika Wilayani Gairo akiwa mgeni rasmi.
Maadhimisho hayo yamefanywa na Vituo vya huduma ya mtoto vilivyopo kwenye makanisa 13 ya Injili yaliyopo Wilaya ya Gairo na Kongwa chini ya "Compassion International Centre".
Katika hotuba yake Mhe. Mchembe aliwakumbusha chimbuko la siku ya mtoto ambapo watoto zaidi ya 2000 waliuwawa na makaburu Kitongoji cha Soweto Afrika Kusini.
Vifo hivyo vilitokana na watoto hao kuandamana wakipinga elimu ikiyokuwa ikitolewa na makaburi kwa mrengo na manufaa ya utawala wa kibaguzi.
Umoja wa Afrika kwa kukumbuka siku hiyo kila mwaka tarehe 16/6 tangu mwaka 1991 wamekuwa wakiadhimisha siku hiyo na Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo.
Mhe. Mchembe alipokea maandamano ya watoto wakiwa na mabango mbalimbali yaliyolenga kufikisha ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2018 " KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUSIMUACHE MTOTO NYUMA".
Mabango hayo, maigizo, ngonjera, mashairi, shuhuda na nyimbo vililenga kufikisha ujumbe wa vilio vya watoto. Maeneo yaliyogusiwa ni kama vile ubakaji, ukawiti, unyanyasaji, ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni.
Mhe. Mchembe alitoa taarifa ya Serikali akieleza jinsi ambavyo Serikali imekuwa mstari wa mbele ikishirikiana na wadau mbalimbali kulinda haki za mtoto hasa wenye mazingira magumu:-
👉 Kutoa elimu bila malipo
👉 Vituo vya Polisi kuunda dawati la jinsia kwa ajili ya wanawake na watoto. Ubakaji, ukeketaji, ulawiti na mimba za utotoni unaripotiwa na kushughulikiwa.
👉 Uundwaji wa dawati la ulinzi na usalama mashuleni, kwenye vitongoji hadi kata.
👉 Wizara kuandaa mwongozo kama nyenzo ya kushughulikia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
Mhe. Mchembe aliwaeleza mikakati ya Wilaya katika kukabiliana na changamoto ya mtoto ikiwemo:-
👉 Mwezi wa nne 2018, Mhe. Mchembe kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama waliunda kamati maalum ya ulinzi na usalama kuchunguza suala zima la mimba za utotoni kuanzia chanzo, visababishi na mikakati ya kulimaliza tatizo hilo.
👉 Kupiga marufuku maridhiano nje ya mahakama na wazazi watakaokamatwa watashughulikiwa.
👉 Elimu kwa wazazi kuepuka lugha zisizofaa kwa watoto.
👉 Kukemea vipigo vinavyopitiliza utu wa mtoto.
👉 Kukamata wazazi wa wanafunzi watoro na wanaobainika kuwazuia watoto wasifanye vizuri wakati wa mitihani.
👉 Kukemea mila potofu hasa ukeketaji na kuoza watoto. Wazazi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hadi sasa kesi zipo Mahakama ya Wilaya ya Kilosa.
👉 Aidha Mhe. Mchembe aliwaasa watoto kujilinda na kulindana. Pia watoe taarifa haraka wanapobaini kufanyiwa vitendo hivyo au mwenzao kufanyiwa.
Katika kuelezea kauli mbiu ya kuelekea uchumi wa viwanda tusimuache nyuma mtoto Mhe. Mchembe alielezea mambo yafuatayo:-
👉 Kwenye sekta ya elimu watoto wanapata elimu bora na sio bora elimu. Serikali ya Magufuli imehakikisha kuna madawati, madarasa, maabara, nyumba za waalimu, kuboresha ufundishwaji pamoja na stadi za kazi.
👉 Malezi bora ni ya wote kuanzia familia, koo, jamii, makanisa na misikiti nk
Toa Maoni Yako:
0 comments: