STAA wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamtwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu tano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.
Hii ni mara ya pili kwa Chidi kukamatwa na madawa ya kulevya mwaka huu mkoani Dodoma huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House.
Hii ni sehemu ya taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa mbaliombali akiwemo Chidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: