JESHI la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rose Manfredy Mndenye ( 31) aliyedaiwa kuuawa na mume wake kwa kile kinachosemekana kuwa ni sababu za wivu wa mapenzi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, leo Jumatatu, Juni 18, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa huyo, John Mwaisango, alikuwa amejificha mkoani Morogoro, hivyo likafanya jitihada za kumnasa na kumtia mikononi mwa dola.
“Baada ya uchunguzi tuliofanya, tumemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mhadhiri wa (UDOM), marehemu Rose Manlfred Mdenye aliyeuawa kwa kukatwakatwa na visu na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake eneo la Swaswa mtaa wa Sarungai.

“Tumemkamata akiwa amejificha katika Kijiji cha Chiwachiwa, Kata ya Mbingu wilayani Ifakara mkoani Morogoro, na sasa mtuhumiwa yupo selo, tunaendelea na uchunguzi zaidi na tukikamilisha tu tutamfikisha mahakamani,” alisema Muroto.

Mhadhiri huyo aliuawa Mei 25 mwaka huu na mtuhumiwa huyo ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la TAG la Swaswa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: