Ratiba ya kusafirisha mwili wa marehemu Mhe. Capt. John Komba itakuwa kama ifuatavyo:
LEO tarehe 02/3/2015 saa 1 asubuhi misa Parokia ya Mt. Bikira Maria Mpalizwa iliopo Mbezi , saa 4 asubuhi mwili utaelekea Karimjee kwa ajili ya kuagwa, na saa 8 mchana mwili utaelekea airport tayari kwa safari ya Songea. Mazishi yatafanyika tarehe 3/3/2015 kijijini kwake Lituhi.
Kufuatia Msiba huu shughuli za kamati hazitakuwepo kwa LEO tarehe 2/3/2015. Ukipata taarifa hii tafadhali mjulishe na mwingine.
IMETOLEWA NA;
OFISI KATIBU WA BUNGE
1.3.2015
Toa Maoni Yako:
0 comments: