Barabara ya Kinondoni Bafra kuja kutokea Best Bite kama mnavyoiona wadau, imekuwa ni kero sana maana nimekuwa ni mashimo ambayo yamejaa maji. Tokea barabara hiyo umejengwa ni takribani miezi sita sasa haijawekewa lami na sisi wananchi hatujui kinachoendelea licha ya kuamka kila siku tunaikuta kama ilivyo. Sasa tunaomba kuuliza manispaa ya Kinondoni imeshindwa kuimalizia barabara hii??? maana ilibaki kuwekewa lami tu lakini cha kushangaza mpaka sasa imeshaharibika tena.
Lori la maji machafu likiwa limenasa baada ya kutumbukia kwenye shimo ambali lilikuwa limejaa maji.
Kondakta wa Lori hilo akihangaika kulinasua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: