Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA), Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung'he waliofika ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akitoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akikabidhi kwa Mh. Lowassa barua ya shukrani kutoka Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA).Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: