Julia Goerges wa Ujerumani akigalagala kwenye uwanja wa vumbi baada ya kuandika historia ya kutwaa taji la Porsche Tennis Grand Prix.
---
---
STUTTGART, Ujerumani
MCHEZA tenisi wa Ujerumani, Julia Goerges juzi aliandika historia baada ya kumchapa nyota namba moja kwa wanawake duniani, Caroline Wozniacki wa Denmark kwa 7-6 (3), 6-3 katika fainali ya Porsche Grand Prix, mjini Stuttgant, Ujerumani.
Julia mwenye miaka 22, aliwahi kutwaa taji moja tu la Bad Gastein, Austria, lakini hili ndilo taji lake la kwanza kubwa linalotambuliwa na chama cha tenisi cha kulipwa ulimwengu (WTA).
Mchezaji huyo ambaye alijiangusha kwa furaha na kugaragara vumbini baada ya mechi hiyo ya fainali kumalizia, anakuwa mchezaji wa kwanza Ujerumani kutwaa taji hilo tangu Anke Huber alipotwaa kwa mara ya mwisho mwaka 1996.
Aidha, ushindi huo umemfanya apande katika kiwango cha ubora kutoka alipo na kuwa namba 27 kwa ubora duniani, katika viwango vipya vilivyotoka jana Jumatatu.
Kwa upande wa wanaume nyota namba moja kwa ubora duniani, Rafael Nadal aliendeleza umwamba wake baada ya kumchapa David Ferrer kwa 6-2, 6-4 na kutwaa tajio la Barcelona Open.
Aidha, ushindi huo ulimfanya Nadal raia wa Hispania kufisha ushindi katika mechi 29 mfululizo kwenye viwanja vya vumbi iki ni rekodi kubwa kwa uhsindi.
Mara ya mwisho Nadal kupoteza mechi kwenye viwanja vya vumbi ilikuwa mwaka 2003, alipochapwa na Mhispania mwenzake Alex Corretja, kwenye michuano hiyo ya Barcelona Open.
Hiyo ni mara ya pili ndani ya muda mfupi kwa Nadal kumchapa Ferrer kwani alimchapa pia katika fainali ya Monte Carlo, Jumapili ya Aprili 17 mwaka huu, ushindi wa juzi umemfanya kufikisha taji la 45 maishani mwake kati ya mataji yanayotambuliwa na ATP.

Toa Maoni Yako:
0 comments: