Na Mwandishi Wetu
Kanisa Katoliki limetangaza rasmi ratiba ya Kipindi cha Kwaresima kwa mwaka 2026, kikianza Februari 18 kwa maadhimisho ya Jumatano ya Majivu na kuhitimishwa Aprili 5 kwa Sikukuu ya Pasaka. Ratiba hiyo inalenga kuwaongoza waumini katika kipindi cha toba, sala na matendo ya huruma kuelekea adhimisho la Ufufuko wa Kristo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 18, 2026 itakuwa Jumatano ya Majivu, siku inayoweka mwanzo wa safari ya siku 40 za Kwaresima. Baadaye, Februari 22 itaadhimishwa Dominika ya Kwanza ya Kwaresima, huku Dominika ya Tano ikiangukia Machi 22 na Dominika ya Matawi kuadhimishwa Machi 29.
Katika Wiki Kuu, Aprili 2 itakuwa Alhamisi Kuu, Aprili 3 Ijumaa Kuu na Aprili 4 Jumamosi Kuu. Hitimisho la kipindi hicho kitakuwa Aprili 5, 2026 kwa maadhimisho ya Pasaka, siku ya furaha kwa Wakristo duniani kote.
Viongozi wa dini wamewahimiza waumini kutumia kipindi hicho kwa kujitafakari, kufunga, kuomba na kuwasaidia wahitaji, wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha imani na mshikamano katika jamii wakati wa safari ya Kwaresima.



Dar es Salaam, Februari 10, 2025 — Kampuni ya Samsung Electronics East Africa imezindua rasmi maduka mawili mapya ya chapa (Brand Stores) katika maeneo ya Kunduchi na Ubungo, ikiwa ni mkakati wa kupanua uwekezaji wake nchini Tanzania na kuimarisha ushindani katika soko la teknolojia na rejareja.
Maduka hayo yamebuniwa kuunganisha bidhaa za simu za mkononi na vifaa vya kielektroniki vya nyumbani chini ya paa moja, yakilenga kuwapatia wateja uzoefu wa moja kwa moja wa mfumo wa bidhaa unaofanya kazi kwa pamoja. Kupitia mpangilio huo, wateja wanapata fursa ya kuona, kujaribu na kuelewa namna simu janja, kompyuta kibao, runinga, vifaa vya kuvaa pamoja na vifaa vya nyumbani vinavyoweza kuunganishwa ili kurahisisha shughuli za kila siku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Kitengo cha Simu za Mkononi wa Samsung Electronics East Africa (Tanzania), Mgope Kiwanga, alisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kampuni katika soko la Tanzania. Alisema maduka hayo yanatoa nafasi kwa wateja kujionea kwa vitendo namna teknolojia ya Samsung inavyoweza kuleta tija katika mawasiliano, burudani na matumizi ya nyumbani.

Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Samsung Tanzania, Daesong Ra, alisema uwekezaji huo unaonesha imani ya kampuni katika ukuaji wa soko la Tanzania na mchango wake katika mageuzi ya kidijitali. Alibainisha kuwa upanuzi huo unachochea ajira, unakuza ujuzi wa wafanyakazi wa ndani na kuongeza upatikanaji wa teknolojia bora kwa watumiaji.
Mbali na kuboresha uzoefu wa wateja, maduka hayo yanatarajiwa kuchangia ukuaji wa uchumi wa ndani kupitia ajira na mafunzo ya kitaalamu kwa Watanzania, huku yakiiweka Samsung katika nafasi imara zaidi ya ushindani katika sekta ya teknolojia inayokua kwa kasi nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KLABU ya Simba SC imemtakia kila la heri mshambuliaji wake, Kibu Denis Prosper, baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Al Nasr SC ya Libya kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu wenye thamani ya dola za Kimarekani 250,000.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba usiku huu, Kibu anaondoka Msimbazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu minne na nusu tangu alipojiunga mwaka 2021 akitokea Geita Gold.
“Baada ya kuwa sehemu ya kikosi chetu kwa misimu minne na nusu, Kibu Denis ‘Mkandaji’ ameuzwa na sasa anakwenda kuanza maisha mapya nje ya Simba SC,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Katika kipindi chake akiwa Simba, Kibu amekuwa mshambuliaji tegemeo akichangia mabao na pasi za mabao katika mashindano ya ndani na kimataifa, huku akisaidia timu kutwaa mataji mbalimbali ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.
Uhamisho wake kwenda Al Nasr unamkutanisha tena na mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala, ambaye tayari alishasajiliwa na klabu hiyo ya Libya mapema.
Hatua hiyo inaonekana kuwa sehemu ya mabadiliko ya kikosi cha Simba kuelekea nusu ya pili ya msimu, huku mashabiki wakimtakia mafanikio mema Kibu katika changamoto yake mpya nje ya Tanzania.
Dar es Salaam, Februari 10, 2026: Katika hatua inayoonesha mwelekeo mpya wa michezo ya kubahatisha nchini, PigaBet imezindua kampeni ya “SHINDA BODA” inayolenga si burudani pekee, bali pia kuwawezesha wachezaji—hasa vijana—kujipatia mtaji wa kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia ushindi wa pikipiki mpya kila wiki.
Kampeni hiyo inawapa wachezaji wawili kila wiki fursa ya kushinda boda boda, zawadi ambayo kwa wengi imekuwa nyenzo muhimu ya kujiajiri au kuongeza kipato cha kila siku. Kupitia mfumo wa PigaPoints, kila mchezaji anayeshiriki michezo ya PigaBet ikiwemo Sports Betting, Casino na Aviator hujikusanyia pointi kwa kila bet au raundi, hali inayoongeza nafasi yake ya kuingia kwenye droo ya ushindi.
Akizungumza kuhusu dira ya kampeni hiyo, Meneja Masoko wa PigaBet, Arthur Kazora, alisema kampeni ya Shinda Boda inalenga kuwafanya wachezaji waone thamani ya muda na ushiriki wao.
“Tumelenga kumwezesha mchezaji kubadili ushindi kuwa fursa ya maisha. Boda si zawadi tu, ni chombo cha ajira, ni mtaji na ni mwanzo wa safari ya kujitegemea kiuchumi,” alisema Kazola.
Tofauti na kampeni nyingi za awali, Shinda Boda imebuniwa kuunganisha burudani, ushindi na uwezeshaji wa kiuchumi. Wachezaji hawazuiliwi na mchezo mmoja pekee, bali wanaruhusiwa kucheza michezo mbalimbali ndani ya jukwaa la PigaBet, jambo linalowawezesha kukusanya pointi zaidi na kuongeza nafasi ya ushindi.
PigaBet pia imeendelea kuvutia wachezaji kwa promosheni zinazolinda na kuongeza thamani ya mchezaji, ikiwemo 10% Cashback kila Jumatatu kwa bet zilizopotea, Win Boost hadi 1000%, pamoja na huduma ya 2UP na Cashout, vinavyompa mchezaji udhibiti zaidi wa michezo yake.
Kwa kutambua nguvu ya mitandao ya kijamii, kampeni hiyo pia imefungua milango kwa content creators kupitia PigaBet Content Creator Challenge, itakayoratibiwa na mshirika wao WAKA.WIN. Kupitia mpango huo, wabunifu wa maudhui watapata nafasi ya kunufaika kifedha kwa kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha kampeni.
Wadau wa michezo ya kubahatisha na vijana kwa ujumla wamehimizwa kujisajili kupitia www.pigabet.co.tz na kushiriki kampeni hiyo, huku PigaBet ikisisitiza umuhimu wa kucheza kwa uwajibikaji kwa watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.
Kwa mtazamo mpya unaoangazia ajira na uwezeshaji, Shinda Boda imejipambanua kama kampeni inayotazama mbali zaidi ya ushindi wa muda mfupi, na kuweka msingi wa matumaini mapya kwa vijana wanaotafuta fursa za kujikwamua kiuchumi.















