Tume ya Ushindani (FCC) imeweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa wakati kwa kutumia mifumo ya kisasa katika utekelezaji wa majukumu yake, ikiwa ni sehemu ya kuongeza ufanisi na uwazi katika huduma za ushindani na biashara nchini.
Akizungumza wakati wa kikao kazi na watumishi wa Tume hiyo kilicholenga kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa, amesema hatua zinazochukuliwa na Tume zinalenga kuwahudumia wananchi kwa viwango vya juu vya ubora vinavyotambulika kitaifa na kimataifa.
Amesema FCC inaendelea kutekeleza dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuwashirikisha wafanyabiashara na wananchi kupitia mifumo rafiki, ya kisasa na yenye ufanisi katika utoaji wa huduma.
Bi. Ngasongwa amebainisha kuwa katika kipindi cha siku 100 za uongozi wa Rais Samia, FCC imechukua hatua za makusudi za kusogeza huduma karibu na wananchi, ikiwemo kuanzisha Ofisi ya FCC Mkoa wa Tanga pamoja na maeneo ya mipakani, hatua iliyolenga kuongeza wigo wa huduma na kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya pembezoni.
Ameongeza kuwa FCC imeendelea kudumisha Cheti cha Ithibati ya Ubora ISO 9001:2015 kutokana na jitihada zake za kutoa huduma kwa weledi, uwazi na kuzingatia viwango vya ubora, huku akiwapongeza watumishi kwa juhudi zao katika kulinda hadhi ya taasisi hiyo.
Katika kikao hicho, watumishi walipata fursa ya kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya Mpango Mkakati Mpya wa Tume wa miaka mitano (2026/27–2030/31), unaoakisi utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050, sambamba na kuimarisha utamaduni wa ushirikishwaji katika maamuzi ya taasisi.
Kikao kazi hicho cha FCC kimefanyika Februari 2, 2026 katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond jijini Dar es Salaam.
Bw. Shalua Magandi, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi akichangia mada wakati wa kikao kazi na watumishi wa Tume, kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond, Jijini Dar es Salaam Februari 02,2026.
Mwenyekiti wa Tughe Tawi la FCC, Bw. Emmanuel Ndyetabula akifuatilia kikao kazi cha Kaimu Mkurugenzi Mkuu na watumishi wa Tume, kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany Diamond, Jijini Dar es Salaam Februari 02,2026.
Ameongeza kuwa kwa sasa ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kila siku, huku akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya kila baada ya miezi mitatu kwa ushauri wa madaktari.Kwa kumalizia, Bibi Clotilda alimshukuru Prof. Shemdoe kwa kukubali kuwasilisha shukrani zake kwa Rais Samia, akisema huruma, upendo na uongozi wa Rais umeokoa maisha yake, na kumuomba aendelee kuwasaidia wananchi wengine wenye uhitaji wa matibabu na huduma muhimu za kijamii.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UN Tourism), Bi. Shaikha Nasser Al Nowais pembezoni mwa mkutano wa Jukwaa la Serikali za Dunia (WGS2026), tarehe 3 Februari, 2026 Madinat Jumeirah, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Bi. Reticia Seni kutoka kampuni ya Dealer Ofisi ya Nganyila Lyapi Sweki, akihudumia wateja (hawapo pichani), waliokwenda kuuza dhahabu zao sokoni.












.jpeg)









.jpeg)












