%20(2).jpeg)
Dar es Salaam, 6 Septemba 2025: Sekta ya usafiri wa anga barani Afrika inaendelea kukua kwa kasi kutokana na ongezeko la utalii, maendeleo ya kiuchumi na kuimarika kwa muunganiko wa kikanda. Takwimu za Julai 23, 2025 zinaonyesha viwanja 10 vya ndege vyenye safari nyingi zaidi za abiria barani humo.
Utafiti huo umebainisha kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Johannesburg (Afrika Kusini) unashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wastani wa safari 249 kwa siku. Ukifuatiwa na Uwanja wa Ndege wa Cairo (Misri) wenye safari 242 na Addis Ababa (Ethiopia) zikiwa 190.
Viwanja vingine vilivyoingia kwenye orodha hiyo ni pamoja na Casablanca (Morocco) safari 114, Nairobi (Kenya) safari 108, Algiers (Algeria) safari 102, Cape Town (Afrika Kusini) safari 102, Lagos (Nigeria) safari 99, Zanzibar (Tanzania) safari 92 na Dar es Salaam (Tanzania) safari 84.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya usafiri, ongezeko hili linaashiria umuhimu wa uwekezaji zaidi katika miundombinu ya viwanja vya ndege na mitandao ya anga ya kikanda ili kuendana na mahitaji yanayoongezeka kila siku.
Sekta hii pia inatajwa kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi, biashara na mawasiliano ya kimataifa, huku ikiendelea kuboresha taswira ya Afrika katika ramani ya usafiri wa anga duniani.


Toa Maoni Yako:
0 comments: