Mkufunzi akiendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea fani ya uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Tumaini Jijini Dar es salaamNA FREDY MGUNDA, DAR ES SALAM.
WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salam idara ya uandishi wa habari wapigwa msasa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kuwaongezea upeo wa elimu ya uandishi wa habari katika nyanja mbalimbali za taaluma hiyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkufunzi wa sheria za vyombo vya habari Adv. Deogratius Bwire alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo wa kuitambua vizuri taalum hiyo ili wakihitimu masomo wanatakiwa kwenda kutumia taalum hiyo kwa kufuata misingi na kanuni walizopewa wakiwa chuoni.
Alisema kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuzijua sheria zilizopo katika sekta ya habari na kuendana na sayansi na teknolojia ambayo imekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara.
“Tunatoa elimu hii kwa lengo la kuongeza uelewa na kwa wanafunzi hao wa vyuo vikuu ili wakihitimu masomo yao waende wakafanye kazi ya uandishi wa habari kwa weredi unaotakiwa kwa kuifanya tansinia hii kuwa imara na yenye wasomi wanaofuata maadili,kanuni,sheria na katiba ya nchi” alisema.
Alisema kuwa waandishi wengi wa habari bado hawazijui sheria mpya za mitandao ya kijamii hivyo waandishi wanatakiwa kusoma kila mara ili kupukana na sheria ambazo zinakuwa zinatungwa kwenye tansia ya habari.
Bwire aliongeza kuwa wananchi wengi hawajui hizi sheria za mitandoa ya kijamii na ndio maana saizi kumetokea kwa wananchi wengi wanapelekwa mahakamani kwa kutukujua sheria hizi za mitandao ya kijamii.
“Kumekuwa na wimbi kubwa hizi karibuni kwa waandishi wa habari wamekumbana na kuanzisha maudhui ya kihabari mtandaoni kinyume cha sheria za mitandaoni ambazo zimetungwa hivi karibuni bungeni na kupitishwa na Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania na sasa zinatumika hivyo umakini unatakiwa sana” alisema
Aliongeza kuwa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa habari mbalimbali kwa lengo la kumsaidia mwandishi wa habari azitambue haki zake na kujitambua mwenyewe kwenye kazi yake.
Kwa upande wake wa mhariri wa Clouds Media Joyce Shebe aliwataka wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari kuwa makini na uandishi wa habari kwa kuhakikisha kuwa wanaandika habari zenye mizani sawa ili kuihabarisha jamii habari ambayo imekamilika.
Shebe alisema kwenye sheria za mitandao inatakiwa kuepuka sana kuonyesha sura za watoto au mtu aliyebakwa au kufanyiwa ukatili kutoonyesha nyuso za wausika ili kulinda haki ya maisha yake.
“Waandishi mkiwa kazini mnatakiwa kufanya za uandishi wa habari kwa kuzingatia maandili ya uandishi ili kuondoa migongano baina ya serikali na jamiii kulingana na aina ya habari ambayo unakuwa umeifanyia kazi” alisema Shebe
Nao baadhi ya wanafunzi chuo cha Tumaini Dar es Salam idara ya uandishi wa habari wamejifunza kwa namna gani wanaweza kupambana na changamoto za tansinia ya habari kutokana naelimu ambayo wamepata kwenye mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa siku tatu katika chuo hicho.
Walisema wanaendelea kujifunza misingi ya wanahabari ili kufanya kazi kwa weredi mkubwa wenye kuzingatia misingi na sheria za taalum hiyo ambayo imekuwa na changamoto nyingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: