Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano huku akielezea furaha aliyonayo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli wa kuleta maendeleo nchini.
Mzee Mwinyi ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati wa Sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo zimefanyika Uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuria na viongozi wa kada mbalimbali na mamia ya wananchi.
Amesema kuwa umoja wetu ni vema Watanzania wakaendelea amani , mshikamano na usalama na kwamba amani linahitaji watu wengi kuliko wanaohitajika kwenye kufanya maovu.
"Katika kulinda amani tunahitajika kuwa wengi lakini kufanya maovu hakuhitaji watu wengi na hao wanaofanya maovu kama wapo basi waache kwani maovu hayana maana,"amesema Mzee Mwinyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: