Articles by "MAGUFULI"
Showing posts with label MAGUFULI. Show all posts
Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na wananchi tayari wamefika katika Uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita tayari kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mwanza wakati wa tukio la kuaga mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza Machi 24, 2021. .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulah, akitoa heshima za mwisho kwa mwili ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza Machi 24, 2021.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akitoa heshima za mwisho kwa mwili ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza Machi 24, 2021. . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 24, 2021.
Mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Machi 24, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho na kuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.John Magufuli ambaye ameagwa leo Machi 20,2021 katika Uwanja wa Uhuru Mkoa wa Dar es Salaam.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ameongoza maelfu ya wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli ambaye ameagwa leo Machi 20,2021 katika Uwanja wa Uhuru.
Dk.Magufuli alifariki dunia Machi 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo na leo kwa mujibu wa ratiba wananchi wa mkoa huo wakiongzwa na Rais Mama Samia wametoa heshima za mwisho kwa mwanamapinduzi na mpenda maendeleo wa Taifa la Tanzania.
Kabla ya Rais Mama Samia kuongoza kutoa heshima za mwisho ilifanyika Misa maalum katioa Uwanja huo wa Uhuru iliyoanza baada ya mwili kuwasili saa 10:13 asubuhi ukitokea Kanisa la mtakatifu Petro (St.Peters') ambako nako ilifanyika Misa ya wafu.
Baada ya Rais Samia kutoa heshima zake kwa Dkt.Magufuli alifuata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aiyekuwa amefuatana na mkewe na baada ya Waziri Mkuu kutoa heshima zake aliondoka uwanjani hapo.Wengine walitoa heshima ni Mama Maria Nyerere,akifuatiwa na Mama Janeth Magufuli aliyeongozona na familia yake.
Viongozi wengine ambao waliotoa heshima za mwisho ni Katibu Mkuu kiongozi Dkt. Bashiru Ally Kakulwa. Rais mstaafu Aman Abedi Karume, majaji wastaafu wakiwamo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalaama.Pia viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Mawaziri pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Baada ya hapo wakafuata wananchi waliokuwa wamesimama katika misururu mirefu.
Awali wakati akiongoza Misa katika Uwanja huo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Tadeus Rweich amewaomba watanzania waliojitokeza viwanjani hapo na waliotazama kupitia televisheni zao majumbani, amumelezea Hayati Dkt. Magufuli ambapo amesema alikuwa ni Rais aliyeipenda nchi yake na alifanya kazi zake Kwa uzalendo mkubwa na Kwa nguvu zake zote.
Amesema Dkt.Magufuli alikuwa ni mtu wa Mungu kweli kwani kila alichokifanya kwake Mungu alikuwa mbele, alijali maslahi ya Taifa na aliwapenda Watanzania kwa vitendo.
Aidha Askofu Rwaich ametoa pole Kwa Rais Mama Samia pamoja na familia ya Hayati Dkt.Magufuli Mama Janeth Magufuli katika kipindi hiki kigumu kuwa mstamilivu na kushikamana na Mungu na kubwa zaidi kumuombea.
Pia ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa Watanzania wote na kuwataka kujipa moyo na matumaini na kwamba yeye hana shaka kwamba Rais Samia atatenda vyema, haki katika shughuli zake mpya majukumu yake.
Salamu za rambirambi.
Bwana Yesu Asifiwe,
Tumsifu Yesu Kristo,
Salaam Aleikum...
MOYO wangu umeugua baada ya kupata taarifa za kifo cha mpendwa wetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea Jumatano ya wiki hii, Machi 17, 2021.
Naomba nichukue fursa hii kutoa POLE zangu kwa mjane wa Rais, Mama Janeth Magufuli, wana familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.
Kifo cha Rais Magufuli niliyemfahamu kwa miaka mingi tangu alipoingia bungeni mwaka 1995 na baadaye tukahudumu wote katika serikali ya marehemu Rais Benjamin Mkapa ni pigo kubwa kwa taifa.
Ninakumbuka namna nilivyofanya naye kazi vizuri na kwa ukaribu na kwa ushirikiano mkubwa wakati Rais Jakaya Kikwete aliponiteua kuwa Waziri Mkuu mwaka 2005.
Mwaka 2015, wote tukiwa wagombea tulishindana kwenye kinyan’ganyiro cha Urais, nilimuona ni mtu mwenye maono na moyo mwema wa kutaka kuliongoza taifa hili, mtu mwenye uthubutu wa kutaka matokeo na Tanzania mpya.
Natambua na kuheshimu uchapakazi wake na namna alivyoweza kurudisha nidhamu ya watumishi wa Serikali na ujasiri wake katika ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu.
Ni wazi kifo cha Rais Magufuli kilichotokea takriban miezi minne tu tangu aingie madarakani katika muhula wake wa pili wa urais kimeliacha taifa katika simanzi kubwa kwa kumpoteza kiongozi shupavu, mzalendo wa kweli, mtetezi wa wanyonge na mchapakazi hodari asiyechoka.
Nitumie fursa kuwaomba Watanzania wenzangu kusimama pamoja na kuliombea taifa amani, umoja na mshikamano wa dhati wakati wote wa kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya kumpoteza jemedari wetu Rais Magufuli.
Si jambo rahisi kwa nchi kumpoteza kiongozi wake mkuu wakati akiwa madarakani.
Kwa sababu hiyo tunapaswa kusimama pamoja na Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kumuombea aweze kusimama imara na kuliongoza taifa kwa weledi na hatimaye kutuvusha salama.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe!
Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu
Subscribe to:
Posts (Atom)