Wachezaji wa Kampuni ya mabasi ya Turu Best kupitia timu zake mbili za Turu na Chico zote zikitokea Manispaa ya Singida mkoani hapa wakimenyana katika Bonanza lililofanyika juzi Uwanja wa Bombardier.
 Bonanza likiendelea.
Bonanza likiendelea.

Na MwandishiWetu

NYASI za Uwanja wa Bombardier ambao huko nyuma ulijulikana zaidi kama ‘Peoples’ juzi nusura ziwake moto baada ya kukanyagwa vilivyo kupitia kandanda safi la Bonanza lililochezwa na vijana wa Kampuni ya mabasi ya Turu Best kupitia timu zake mbili za Turu dhidiya Chico zote zikitokea Manispaa ya Singida mkoani hapa.

Kilichovutia zaidi mbali ya namna matajiri wa mabasi hayo walivyojumuika kwa furaha pamoja na wafanyakazi hao, lakini kikubwa ni viwango vya soka vya hali ya juu vinavyoonyeshwa mithiri ya kabumbu za mechi mbalimbali zileza Ligi Kuu ambazo tumezoea kuzitazama.

Kama nimara yako ya kwanza kutazama bonanza hilo kwa ubora wake na namna wachezaji wa timu zote wanavyosakata kabumbu na amini itakuwa ni vigumu kwako kuamini kama walindamilango wa timu hizo yaani Turu Best na Chico nimafundigereji, na washambuliaji wake ni madereva maarufu tena ni wale wa usukani wa mabasi makubwa na sio bajaji, na kiungo mkabaji ni mkatishaji tiketi kutoka Kampuni ya Usafirishaji abiria ya Turu Best.

Ni vigumu sana kutofautisha mchezaji wa Turu au Chico na wale wanaochezeaLigiKuu, kama huamini sogea viwanja vya Bombardier hapa Singida kila Jumapili utakachoshuhudia kamwe huwezi kuamini-ni zaidi ya vipaji tena adimu vilivyofichika.

Kandanda safi baina ya timu ya Turu Best iliyopo maeneo ya Uteminidhidi ya Chico yenye makao yake eneo la Kindai, zote zikitokea Manispaa ya Singida mkoani hapa lilianza kwa kasi majira ya saa 11 jioni kwa timu zote kutunishiana misuli, huku mashabiki mara kadhaa wakisikikaw akipiga yowe kumlaumu mwamuzi wa mchezo huo kwa kuonyesha wazi wazi kuwabeba Turu.

Dakikaya 19 kipindi cha kwanza Chico ilipata penati kufuatia mlinzi wa Turu Best Majombi Nurdin kumshika bukta kwa nyuma na kuivuta hadi kumwangusha mshambuliaji wa Chico eneo la hatari, lakini hata hivyo kiungo wa Chico Faidh Mohamed alipiga nje penati hiyo.

Kasiyamchezo iliyoambatana na mawingu ya mvua ilipelekea kufanyika kwa mabadiliko ndani ya kikosi cha chico dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza, ambapo alipumzishwa jezi namba 7 Mweusi wa Weusi na kuingia Cosmas Komanga ‘maarufu Mzee Cosma,’ lakini hadi mapumziko hakuna timu iliyo ona goli la mwenzake.

Kipindi cha pili Turu Best waliingia kwa kupania, huku makelele ya mashabiki walioonyeshakuishangilia zaidi Chico yakionyesha kuwachanganya na dakika 60 ya mchezo mshambuliaji wa Turu alipiga shuti kali lililogonga mwamba na kurudi ndani, hali iliyo wafanya chico kucharuka kama mbogo na hatimaye dakikaya 70 mshambuliaji wa chico Hasan Hasan aliwanyanyua kwa shangwe mashabiki kwa kufunga bao la kuongoza.

Mlindamlango wa Chico Juma Mlali alizawadiwa kadi ya njano kwa utovu wa nidhamu, kosa la kujivuta-vuta kwalengo la kupoteza muda hali iliyowashtua wachezaji wa chico kuongeza kasi na hatimaye dakikaya 85 mshambuliaji wa timu hiyo Faidh Mohamed alijikuta akifuta makosa yake ya kukosapenati hapo awali na kupachika bao safi lililoipeleka Chico kileleni zaidi kwa idadiya mabao 2.

Hadi dakika 90 zamchezo huo ulioambatana na mvua kali muda mfupi kabla ya kumalizika timu ya Chico kutoka Kindai iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidiya wapinzani wao watoto wa Utemini Turu Best.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: