TRENDING NOW






Hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imeondokana na changamoto ya kukatiza baadhi ya huduma za matibabu kama upasuaji na pindi umeme unapokatika baada ya Bohari kuu ya dawa MSD kukabidhi jenereta lenye thamani ya shilingi milioni 65 itakayotumika kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameagiza uongozi wa hospitali ya Halmashauri hiyo kutenga bajeti ya mafuta ya jenereta hilo ili litumike wakati wowote pindi umeme unapokatika. 
"Niwaombe viongozi mjipange ili hili jenereta mlilopewa liwe linafanyakazi kwa ufasaha, tengeni bajeti ya mafuta ili pindi umeme unapokatika linawaka na mambo yanakwenda vyema," amesema RC Sendiga.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano mjini Kibaya wilayani Kiteto, meneja wa MSD kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa amesema jenereta hilo lenye uwezo wa KVA 75 ni sehemu ya mahitaji ya vifaa vya afya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 699 vilivyoagizwa na hospitali hiyo kwa bohari kuu ya dawa MSD katika mwaka wa fedha 2023/2024. 


 Amesema tayari MSD imeshakabidhi vifaa vingine vilivyoagizwa katika hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 683 sawa na asilimia 98 ya vifaa vilivyoagizwa na halmashauri hiyo kupitia MSD na ameahidi wakati wowote kuanzia sasa kukamilisha sehemu iliyobaki ambayo ni mfumo wa kuhifadhi miili (mortuary cabinet). 
Jenereta lenye thamani ya shilingi milioni 65.

Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt Vicent Gyunda ameshukuru bohari kuu ya dawa kanda ya Dodoma kukabidhi jenereta hilo kwa wakati ambayo sasa itawezesha uhakika wa huduma za upasuaji wa wagonjwa, kuwapa joto watoto njiti pamoja na huduma ya kuhifadhi maiti. 

Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa maeneo ambayo huduma ya umeme hukatika kila mara kutokana na uchakavu wa miundombinu hali ambayo imekiwa ikitatiza utoaji wa huduma za kitabibu zinazohitaji uwepo wa umeme katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya hiyo mjini Kibaya.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mh. Mudrick Soraga (kulia), akimsikiliza Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Shani Kinswaga, wakati wa kongamano la Z-Summit 2025 lililofanyika katika Chuo Kikuu cha SUZA, Zanzibar. Kongamano hilo la kila mwaka, lililofanyika kuanzia Februari 19-20, liliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ili kujadili changamoto na suluhisho za kuendeleza Zanzibar kama moja ya maeneo bora ya utalii duniani.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

Zanzibar, Tanzania – Benki ya Exim Tanzania imeimarisha dhamira yake ya kukuza na kuendeleza sekta ya utalii Zanzibar kwa kushirikiana na wadau muhimu wa sekta hiyo, wakiwemo Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), ili kuwezesha waendeshaji wa shughuli za utalii kufanya malipo kama ada za kuingia kwenye hifadhi kwa haraka, kwa usalama na kwa urahisi.

Mkutano wa Z-Summit 2025, uliofanyika katika Chuo Kikuu cha SUZA, Tunguu, uliwakutanisha wadau wa serikali, wafanyabiashara, na wadau wa sekta ya utalii na ukarimu ili kujadili suluhisho bunifu za kuboresha nafasi ya Zanzibar kama moja ya vivutio bora vya utalii duniani.  
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Shani Kinswaga, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisisitiza safari ya benki hiyo na Z-Summit tangu kuanzishwa kwake, akieleza kuwa huu ni mwaka wa tatu mfululizo wa udhamini wao katika mkutano huo.  

“Mkutano huu ni jukwaa muhimu la kushirikiana, kubadilishana maarifa na kujadili mikakati ya kuimarisha zaidi nafasi ya Zanzibar kama moja ya vivutio bora vya utalii duniani. Uungwaji mkono wa Benki ya Exim unaonesha imani yetu thabiti katika sekta ya utalii kama kiini cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii,” alisema Kinswaga.  

Kinswaga alielezea juhudi za benki hiyo katika kutumia teknolojia kutoa suluhisho rahisi za kifedha zinazokidhi mahitaji ya biashara za utalii. Kwa kuongezeka kwa mahitaji ya miamala ya kidigitali, Benki ya Exim imeanzisha huduma bunifu za kibenki, zikiwemo kutumia simu, kadi, na mifumo ya malipo mtandaoni, ili kuhakikisha ufanisi, usalama, na urahisi kwa wafanyabiashara na watalii.  
Akizungumzia ushirikiano wao na TANAPA, Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Benki ya Rejareja wa Benki ya Exim, alisema, “Katika Benki ya Exim, tunatambua kuwa ufanisi, usalama, na urahisi ni muhimu katika sekta ya utalii. Ndiyo maana tumeshirikiana na wadau kama TANAPA na NCAA kuwezesha malipo yasiyo ya fedha taslimu kwa huduma mbalimbali, ikiwemo ada za kuingia kwenye hifadhi. Akaunti ya Waendeshaji wa shughuli za Utalii inajumuisha Kadi ya Exim TANAPA, iliyoundwa mahsusi kurahisisha miamala katika maeneo yote ya hifadhi nchini Tanzania.”  

Katika kuthibitisha dhamira yake ya kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha, Benki ya Exim ilitangaza mpango wake wa kuendelea kupanua huduma zake Zanzibar. Ikiwa tayari na matawi mawili yanayofanya kazi, benki hiyo ina mpango wa kufungua matawi katika maeneo mengine ya kimkakati. Hii inaonesha azma ya Benki ya Exim ya kusogeza huduma za kibenki karibu na biashara, ikiwawezesha kupata suluhisho za kifedha zinazosaidia maendeleo ya miundombinu, ukuaji wa biashara, na ufanisi wa uendeshaji.  

Kadri mazingira ya utalii yanavyoendelea kubadilika, Benki ya Exim inasalia kuwa mshirika wa kuaminika wa kifedha kwa biashara zinazotaka kupanuka, kuboresha huduma zao, au kuwekeza katika fursa mpya. Suluhisho zake maalum za kifedha zimeundwa kusaidia kupata rasilimali zinazohitajika ili kustawi katika soko lenye ushindani.  

Kupitia ushirikiano imara, matumizi ya teknolojia za kidigitali, na upanuzi wa huduma zake, Benki ya Exim haitoi tu msaada kwa sekta ya utalii bali pia inachangia katika maendeleo ya uchumi wa Zanzibar kwa ujumla. Ushiriki wa Benki ya Exim katika mkutano wa Z-Summit 2025 ni uthibitisho wa dhamira yake isiyotetereka ya kusaidia ukuaji endelevu wa sekta ya utalii Zanzibar. 

Kwa kushirikiana na wawekezaji, wafanyabiashara, na mamlaka za serikali, benki hiyo inaunda mustakabali ambapo utalii utaendelea kuwa kichocheo cha maendeleo ya uchumi, kuongeza ajira, na kuifanya Zanzibar kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka kote ulimwenguni.  
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza tarehe 18 hadi 19 Februari, 2025 Mkoani Morogoro . Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani humo linataraji kuanza Machi mosi 2025 na kufikia tamati Machi 07,2025 huku vituo vikitaraji kufunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:jioni kwa siku zote saba.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza tarehe 18 hadi 19 Februari, 2025 Mkoani Morogoro . Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani humo linataraji kuanza Machi mosi 2025 na kufikia tamati Machi 07,2025 huku vituo vikitaraji kufunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:jioni kwa siku zote saba.

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba za kufunga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Ndg. Kailima R. K wakati wa kufunga mafunzo hayo. Mwenyekiti wa Mafunzo ambaye pia ni Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Ndg. Emmanuel Vuri akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Meza kuu ikimsikiliza Mwenyekiti wa mafunzo.

Mjumbe Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira akiwa wakati wa kufunga mafunzo hayo. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Ndg. Kailima R. K akizungumza jambo na washiriki.


Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba za kufunga.
******************Na. Mwandishi Wetu
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari; la Kudumu la Wapiga Kura wameaswa kutekeleza majukumu waliyopewa kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omari Ramadhan Mapuri wakati akifunga mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa daftari mkoani Morogoro leo Machi 19, 2025.

“Mnapaswa kutekeleza majukumu mliyopewa kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume,” amewaasa watendaji hao ambao wamehudhuria mafunzo ya siku mbili.

Balozi Mapuri ametoa wito kwa watendaji hao kuendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote waliyopewa ili kuongeza uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao wakati wa kutekeleza zoezi lililopo mbele yao.

Akifunga mafunzo kama hayo mkoani Tanga, Mjumbe wa Tume ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari amewataka watendaji hao kusoma katiba na sheria ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Someni kwa makini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Uchaguzi, Kanuni za uboreshaji, Maelekezo na Miongozo yote inayotolewa na Tume ili kazi yenu ifanyike kwa unadhifu na haki,” amesema.

Jaji Asina amewakumbusha watendaji hao juu ya wajibu wao wa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao kwenye uchaguzi mkuu utakoafanyika mwaka huu.

Uboreshaji wa Daftari utafanyika mkoani Morogoro na kwenye Mkoa wa Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga kwa siku saba kuanzia tarehe 01 hadi 07 Machi, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli( PURA) wakati wa Kikao cha Baraza hilo linalofanyika tarehe 18 na 19 Februari 2025, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi. Charles Sangweni (kushoto). Kulia ni Katibu wa Baraza Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Ebeneza Mollel,wakati wa Kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mpango na Bajeti hilo linalofanyika tarehe 18 na 19 Februari 2025, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakati wa Kikao cha Baraza hilo linalofanyika tarehe 18 na 19 Februari 2025, mkoani Morogoro. Kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi. Charles Sangweni.
---------
*Ataka Duru ya Tano ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kuwa na matokeo chanya

*Aipongeza PURA kuwashirikisha Watumishi kujadili mipango ya Bajeti ya Taasisi

MOROGORO

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli( PURA) kuendelea kuvutia uwekezaji katika vitalu vilivyo wazi vya mafuta na gesi asilia ili kuongeza kiasi cha nishati hiyo nchini.

Mhe. Kapenga amesema hayo leo wilayani Morogoro, Mkoa wa Morogoro wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa PURA kinacholenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemoMpango na Bajeti ya Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26.

” Mkifanikiwa kuvutia uwekezaji katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi, nchi itaongeza ugunduzi wa rasilimali hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na kuogeza futi za ujazo wa gesi inayopatikana nchini, Pia mkiendelea kuvutia uwekezaji kupitia Duru ya Tano ya kunadi vitalu itakayozinduliwa mwezi machi mwaka huu, pamoja na faida zilizopo, mtakuwa mmeendeleza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuifungua Tanzania kiuchumi na kuvutia uwekezaji zaidi.”Amesema Kapinga.

Amesema Wizara ya Nishati inatambua umuhimu wa tukio la Duru ya Tano ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini pamoja na kutambua kazi kubwa ambayo imeshafanyika kuelekea uzinduzi wa tukio hilo ambalo amesema kuwa ni muhimu katika

kuvutia uwekezaji zaidi katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.

“ Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukizungumzia ugunduzi wa futi za ujazo trilioni 57.54 pekee ni wakati sasa wa kufanya zaidi na zaidi ili tuweze kuongeza ugunduzi wa rasilimali hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa.” Amesisitiza Mhe.Kapinga

Katika kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi, ameupongeza uongozi wa PURA kwa kuendelea kuwashirikisha watumishi wake katika kujadili, kupanga na kupitisha mipango na Bajeti ya Taasisi kwenye Baraza la Wafanyakazi ikiwa ni utekelezaji pia wa Sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma.

Amesema kufanyika kwa vikao hivyo ni ishara tosha ya utawala bora mahala pa kazi kwa kuwa watumishi wanapata fursa ya kuchangia mawazo yao kuhusu hali ya uendeshaji wa Taasisi hivyo kuendelea kuwa ni sehemu muhimu ya Taasisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli( PURA) Mhandisi. Charles Sangweni, amesema duru ya tano (5) ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na

gesi asilia nchini inatarajiwa kuzinduliwa mwezi Machi, 2025 Jijini Dares salaam wakati wa Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki (EAPCE’25).

Amesema PURA inaendelea kusimamia na kudhibiti shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa gesi asilia katika vitalu mbalimbali nchini na Kuhakikisha watanzania wazawa wanashirikishwa katika miradi mbalimbali ya mkondo wa juu wa petroli nchini.
Dar es Salaam. Tarehe 18 Februari 2025: Ikiwa katika maadhimisho ya miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, Benki ya CRDB imetangaza mafanikio makubwa ya hatifungani ya miundombinu ya ‘Samia Infrastructure Bond,’ ambayo imevuka lengo kwa asilimia 115, ikikusanya Shilingi bilioni 323 - zaidi ya mara mbili ya lengo lake la awali la kukusanya Shilingi bilioni 150.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ameipongeza Benki ya CRDB kwa mafanikio makubwa ya mauzo ya Hatifungani ya Samia Infrastructure Bond iliyokusanya TZS bilioni 323 ambazo ni zaidi ya mara mbili ya lengo la awali la kupata TZS bilioni 150.
Mafanikio haya yaliyopatikana ndani ya mwezi mmoja na nusu wa mauzo hayo yanaonyesha imani kubwa waliyonayo wawekezaji kwa Benki ya CRDB hali inayoiweka mahali pazuri zaidi kuimarisha nafasi yake kama benki kinara katika sekta ya fedha nchini.

Hatifungani hii iliyotajwa kwa heshima ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaonyesha dhamira ya Benki ya CRDB kuchangia kukuza uchumi wa taifa na kuimarisha kipato cha mwananchi mmojammoja.

Kupitia fedha zilizokusanywa baada ya mauzo ya hatifungani hii, wananchi watanufaika kutokana na ukamilishaji kwa wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya barabara za mijini na vijijini.
Mheshimiwa Mchengerwa amesifu mafanikio haya akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji nchini.

“Hatifungani ya Samia Infrastructure Bond ni mfano halisi wa namna ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unavyoweza kuleta manufaa kwa taifa letu. Kiasi hiki cha TZS 323 bilioni kilichokusanywa kinatoa mwanga wenye matumaini kwa maendeleo ya miundombinu hasa ya barabara huko mbeleni.
Nawapongeza sana Benki ya CRDB kwa ubunifu huu mliokuja nao katika kuisaidia serikali kukamilisha mipango yake ya kuboresha maisha ya wananchi,” amesema Waziri Mchengerwa.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu tangu tarehe 29 Novemba 2024 uzinduzi wa mauzo hayo ulipofanyika mpaka Januari 17 dirisha hilo lilipofungwa, kampuni na taasisi 327 zimejitokeza kuwekeza zaidi ya TZS 118.99 bilioni pamoja na watu binafsi 6,896 waliowekeza jumla ya TZS 204.1 bilioni. Asilimia 94 ya kiasi chot ekilichopatikana kimekusanywa kupitia Programu ya SimBanking.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema mafanikio yaliyoyapata yanadhihirisha ukubwa nauwezo wa uwekezaji walionao wananchi pamoja na kampuni zilizopo katika soko letu sambamba na utayari wao kuwekeza hasa wanapojiridhisha na uhakika wa mradi na Benki ya CRDB inajisikia fahari kubwa kuaminiwa na Watanzania kwa ujumla wao.

Kazi kubwa iliyofanywa na menejimenti ya Benki ya CRDB ikishirikiana na Wizara ya TAMISEMI kupitia Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) amesema imekuwa na mafanikio makubwa ambayo matunda yake yatawanufaisha Watanzania wengi. “Tumepata wawekezaji wengi binafsi kwa sababu walimudu kiwango cha chini cha shilingi 500,000 tu.
Fedha zote tulizozikusanya kwenye mauzo ya hatifungani ya Samia Infrastructure Bond zitatumika kuwawezesha makandarasi wa wanaotekeleza na watakaoshinda zabuni zitakazotangazwa na TARURA. Tunaamini upatikanaji wa fedha hizi utasaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha miradi kwa wakati,” amesema Nsekela.

Wawekezaji hawa, Nsekela amesema wataendelea kushirikiana nao kwa kipindi chote cha miaka mitano ya uhai wa hatifungani hii kama walivyowaahidi wakati wa mauzo yaliyofanyika nchi nzima ikiwamo kulipa riba ya asilimia 12 kwa mwaka itakayotolewa kwa awamu nne. “Malipo ya riba yatakuwa yanafanyika kila tarehe 10 Februari, 10 Mei, 10 Agosti, na 10 Novemba. Kwa mwaka huu, wataanza kupokea malipo ya faida tarehe 10 Mei,” amesema Nsekela.

Hatifungani ya Samia Infrastructure Bond ni awamu ya pili ya Mpango wa Muda wa Kati wa Miaka Mitano kwa ajili ya kukusanya Shilingi za Kitanzania sawa na Dola za Marekani Milioni 300 ambao uliridhiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Fedha na Mitaji (CMSA) mwaka 2023.
Kupitia mpango huo, mwaka 2023 Benki ya CRDB ilikuwa ya kwanza nchini kuzindua hatifungani ya kijani iliyopewa jina la ‘Kijani Bond’, ambayo ilikuwa hatifungani ya kwanza kwa ukubwa kusini mwa Jangwa la Sahara. “Kijani Bond ilikuwa ni awamu ya kwanza ya mauzo ya Mpango wa Muda wa Kati wa Miaka Mitano na Samia Infrastructure Bond ni awamu ya pili ya mpango huo.

Kama tulivyovuka lengo katika mauzo ya Hatifungani ya Samia Infrastructure Bond, hali ilikuwa hivyo pia kwenye Kijani Bond iliyotuwezesha kukusanya shilingi bilioni 171.82 kutoka shilingi bilioni 40 zilizokusudiwa sawa na ufanisi wa asilimia 429.6,” amefafanua Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA, Mhandisi Victor Seff amesema ushirikiano huu ulioanzishwa kati ya Benki ya CRDB na TARURA utakuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji wa miradi ya barabara nchini. “Tunayo miradi mingi inayotekelezwa katika maeneo tofauti nchini na changamoto kubwa iliyokuwepo ilikuwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya malipo ya makandarasi. Naamini wengi sasa watapata fedha zao kwa wakati ili kukamilisha miradi kwa muda uliopangwa,” amesema Mhandisi Seff.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CMSA, CPA Nicodemus Mkama alisema kuwa kuorodheshwa kwa Samia Infrastructure Bond kumetongeza thamani ya uwekezaji katika hatifungani za kampuni na taasisi kwa asilimia 38.9, na kufikia TZS trilioni 1.16 kutoka TZS bilioni 837.31.

"Samia Infrastructure Bond ni kielelezo wazi cha nguvu za masoko yetu ya mitaji, na kuufanya Soko la Hisa la Dar es Salaam kuwa mchezaji muhimu katika kuwezesha uwekezaji katika miradi ya miundombinu ya kitaifa ya Tanzania," aliongeza Bwana Mkama.

Baada ya kutangaza matokeo ya mauzo, hatifungani hiyo iliorodheshwa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kuwaruhusu wawekezaji waliochelewa kupata nafasi ya kushiriki kuijenga nchi yao huku wakipata faida ya asilimia 12 itakayotolewa kwa kipindi chote cha miaka mitano.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Peter Nalitolela amesema kila siku idadi ya Watanzania wanaoshiriki sokoni hapo inazidi kuongezeka jambo linalotia matumaini kwamba litazidi kukua hivyo kuwa na manufaa makubwa hapo siku za mbeleni. “Mafanikio zinazopata makampuni yaiyoorodheshwa sokoni ni mfanikio ya soko zima.

Sisi wasimamizi wa soko tunapata faraja kuona mambo yanaenda vizuri kila kunapokuwa na bidhaa mfano wa Hatifungani hii ya Samia Infrastructure Bond ya Benki ya CRDB,” amesema Nalitolela.




Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa siku saba.Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa siku saba.





Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa siku saba.

Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume, Ndg. Stanslaus Mwita akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo hayo.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani wakati wa mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro unaotaraji kuanza kufanyika Machi 01 hadi 07, 2025. Vituo vikifunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni kwa siku saba.
Onesho la vitendo la uandikishaji likifanywa na wataalam kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.


Washiriki mbalimbali wakiwa katika mkutano huo mkoani Morogoro.
 
********************** 
Na. Mwandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanza kwa mzunguko wa 12 wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utafanyika mkoani Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga kwa siku saba kuanzia tarehe 01 had 07 Machi, 2025.

Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Morogoro leo tarehe 17 Februari, 2025, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huo utafanyika kwenye mkoa huo na mkoani Tanga kwenye halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga.

“Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 12 kati ya mizunguko 13 ya uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu wa 12 unahusisha Mkoa huu wa Morogoro na Mkoa wa Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema mikoa 27 tayari imekamilisha zoezi hilo ambayo ni pamoja na Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma na Singida.

Ameitaja mikoa mingine kuwa ni Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

“Mikoa miwili ya Pwani na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza inatarajia kukamilisha zoezi hilo tarehe 19 Februari, 2025,” amesema.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndugu. Kailima Ramadhani amesema Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 302,752 mkoani Morogoro sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 1,612,952 waliokuwepo kwenye daftari la wapiga kura mwaka 2020.

“Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Morogoro utakuwa na wapiga kura 1,915,704. Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha,” amesema.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Morogoro una vituo 2,816 vitakavyotumika kwenye uboreshaji wa daftari ikiwa ni ongezeko la vituo 112 katika vituo 2,704 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.