Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka, akikagua miundombinu ya barabra iliyoharibiwa na mvua kubwa iliyonyesha wilayani humo.
Na Dotto Mwaibale
Uongozi ni dhamana aliyopewa kiongozi husika kwa ajili ya kusimamia shughuli za maendeleo pamoja na changamoto mbalimbali za wananchi zinapo jitokeza na siyo kukaa ofisini na kuwatuma au kuwaagiza wakuu wa idara kwenda kuzishughulikia.
Disemba 26 2025 mvua kubwa zilinyesha katika Tarafa ya Kidete wilayani Kilosa mkoani Morogoro na kuharibu baadhi ya miundombinu ya barabara na mashamba na kuwaacha wananchi wasijue la kufanya.
Kutokana na wilaya hiyo kuwa na kiongozi bora na mchapakazi ambaye anaguswa na changamoto za wananchi Desemba 30, 2025 Mkuu wa wilaya hiyo Shaka Hamdu Shaka akimbatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya bila ya kuchelewa walienda kukagua maeneo yote yaliyoathirika na mvua hiyo ili kuona ukubwa wa changamoto hiyo ili Serikali iifanyie kazi na maisha ya wananchi yaendelee kama kawaida baada ya miundombinu iliyoharibiwa na mvua hiyo kurekebishwa.
Mvua hiyo iliyoambatana na upepo imesababisha athari kwa wakazi wa kata mbili za Dumila na Magole ikiwa ni pamoja na nyumba za makazi na biashara kuathiriwa pamoja na baadhi ya miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na baadhi ya taa za barabarani.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka aliyetembelea maeneo yalioathirika na mvua hizo alisema serikali inafanya tathmini ya haraka ili kujua athari zilizojitokeza.
DC Shaka alisema kuwa zaidi ya nyumba 120 zikiwemo za makazi pamoja na maghala mawili ya kuhifadhia nafaka yamekumbwa na maafa hayo.
Aidha amesema kuwa mpaka sasa hakuna athari ya kibinadamu iliyojitokeza kutokana na upepo huo huku akitoa wito kwa wananchi wote wa kilosa kuchukua taadhari kipindi hiki cha mvua.
Ukaguzi wa maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ukiendelea.
Kazi ikiendelea.


Toa Maoni Yako:
0 comments: