Na Mwandishi Wetu

Rais wa Kenya, William Ruto, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ol Kalou, David Njuguna Kiaraho, akieleza kusikitishwa kwake na msiba huo alioutaja kuwa pigo kubwa kwa taifa.

Kupitia ujumbe wake, Rais Ruto amesema mawazo na maombi yake yako pamoja na familia ya marehemu, marafiki pamoja na wananchi wa Ol Kalou katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Akimzungumzia marehemu Kiaraho, Rais Ruto alimtaja kuwa kiongozi mnyenyekevu, thabiti na mwenye maono, aliyekuwa nguzo muhimu kwa jamii yake kutokana na kujitolea kwake kuwatumikia wananchi wake kwa dhati.

Aliongeza kuwa marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu pamoja na utumishi wake uliotukuka ndani ya Bunge la Taifa, ambako alisimamia maslahi ya wananchi wake kwa uadilifu.

Rais Ruto pia alibainisha kuwa maisha ya marehemu ni funzo kwa viongozi wa kizazi cha sasa, akiwahimiza kuweka mbele huduma kwa wananchi badala ya siasa zisizo na tija, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza kaulimbiu yake ya “Kazi Kwanza, Siasa Baadaye.”

Amehitimisha kwa kutoa pole na kumuombea marehemu apumzike kwa amani, huku taifa la Kenya likiendelea kuomboleza kiongozi huyo aliyegusa maisha ya wengi.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: