Na Mwandishi Wetu.
Dodoma, Machi 30, 2026 — Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, Alex Sospeter Mkama, amekabidhiwa rasmi ofisi ya kuongoza kamisheni hiyo katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dodoma.
Hafla hiyo ya makabidhiano imeongozwa na aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ulrich Matei, ambaye alimkabidhi majukumu hayo kwa utaratibu rasmi, akimtakia mafanikio mema katika uongozi wake mpya.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi, CP Mkama alieleza dhamira yake ya kuendeleza juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, akisisitiza umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu katika kudumisha amani na usalama nchini.
Kwa upande wake, DCP Matei alisema kuwa ana imani uongozi mpya utaongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamisheni ya Polisi Jamii, hasa katika kujenga uhusiano chanya na wananchi na kushughulikia changamoto za kiusalama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.




Toa Maoni Yako:
0 comments: