Mhe. Anne Samamba Makinda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Bw. Jaffer Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Dkt. Albina Andrew Chuwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
Prof. Makenya Abraham Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Dar es Salaam, Februari 11, 2026 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali za taasisi za umma katika hatua inayolenga kuimarisha ufanisi na usimamizi wa taasisi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, walioteuliwa ni pamoja na Mhe. Anne Samamba Makinda ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Katika uteuzi huo, Bw. Jaffer Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), akichukua nafasi ya Bw. Ally Amani Karavina. Aidha, Dkt. Albina Andrew Chuwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).

Rais pia amemteua Prof. Makenya Abraham Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), taasisi inayosimamia elimu ya juu nchini.

Uteuzi huo unaanza mara moja na unatarajiwa kuongeza nguvu katika usimamizi, uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: