Na Mwandishi Wetu
Kanisa Katoliki limetangaza rasmi ratiba ya Kipindi cha Kwaresima kwa mwaka 2026, kikianza Februari 18 kwa maadhimisho ya Jumatano ya Majivu na kuhitimishwa Aprili 5 kwa Sikukuu ya Pasaka. Ratiba hiyo inalenga kuwaongoza waumini katika kipindi cha toba, sala na matendo ya huruma kuelekea adhimisho la Ufufuko wa Kristo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 18, 2026 itakuwa Jumatano ya Majivu, siku inayoweka mwanzo wa safari ya siku 40 za Kwaresima. Baadaye, Februari 22 itaadhimishwa Dominika ya Kwanza ya Kwaresima, huku Dominika ya Tano ikiangukia Machi 22 na Dominika ya Matawi kuadhimishwa Machi 29.
Katika Wiki Kuu, Aprili 2 itakuwa Alhamisi Kuu, Aprili 3 Ijumaa Kuu na Aprili 4 Jumamosi Kuu. Hitimisho la kipindi hicho kitakuwa Aprili 5, 2026 kwa maadhimisho ya Pasaka, siku ya furaha kwa Wakristo duniani kote.
Viongozi wa dini wamewahimiza waumini kutumia kipindi hicho kwa kujitafakari, kufunga, kuomba na kuwasaidia wahitaji, wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha imani na mshikamano katika jamii wakati wa safari ya Kwaresima.



Toa Maoni Yako:
0 comments: