Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akili (Wa pili kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Jafari Matundu (Wa pili kushoto)wakikata utepe kama ishara ya kufungua kwa tawi jipya la Benki hiyo Paje, linalolenga Kusogeza huduma kwa wananchi na wafanya Biashara wa eneo hilo na kusaidia katika kukuzaUtalii na uchumi wa buluu wa Zanzibar. Tukio hilo limeshudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Bunafsi wa Benki ya Exim TanzaniaAndrew Lyimo (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mhe. Othman Ali Maulid (kulia).Hafla hiyo imefanyika tarehe 21 Februari 2026 Visiwani Paje Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu.

Zanzibar, Februari 21, 2026 — Benki ya Exim Bank Tanzania imezindua rasmi tawi jipya katika eneo la Paje ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa visiwa hivyo, hususan sekta ya utalii.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akili, pamoja na viongozi wa Serikali, taasisi za fedha, sekta binafsi na wadau wa maendeleo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Jaffari Matundu, alisema kufunguliwa kwa tawi hilo ni hatua muhimu katika kuimarisha ujumuishi wa kifedha na kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
Alisema uwepo wa tawi hilo utaongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wawekezaji wa utalii, wajasiriamali, wavuvi na wafanyabiashara wadogo na wa kati, huku pia likitoa suluhisho za kidijitali na huduma za ufadhili wa biashara.

Kwa upande wake, Dkt. Akili alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi wa Zanzibar kwa kuwa huduma za kifedha zilizo karibu na wafanyabiashara na wawekezaji huchochea biashara, ajira na mapato ya wananchi.
Mbali na huduma za kifedha, benki hiyo imeendelea kutekeleza miradi ya uwajibikaji kwa jamii kupitia mpango wake wa Exim Cares, ikichangia katika sekta za afya, elimu na mazingira. Miongoni mwa miradi hiyo ni msaada kwa taasisi za afya ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na miradi ya elimu na usalama wa jamii Zanzibar.

Uzinduzi wa tawi hilo unaimarisha nafasi ya benki hiyo kama mshirika wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku ukilenga kuchochea ukuaji wa biashara, uwekezaji na ustawi wa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: