Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Benki ya Stanbic, Dickson Senzi (kushoto), na Meneja wa Kidijitali na Biashara Mtandaoni wa benki hiyo, Godlisten Shirima (kulia), wakimuonyesha Malipula Suti (katikati) jinsi ya kupokea malipo kupitia LIPA SIMPO na kusisitiza kasi, usalama na gharama nafuu ya suluhisho za malipo ya kidijitali za Stanbic kwa biashara za ndani. Ziara ya kutembelea maduka yanayotumia huduma hiyo lilifanyika jijini Dar es salaam jana.
Mkuu wa Idara ya Kidijitali na Biashara Mtandaoni Benki ya Stanbic Tanzania, Edward Balandya (watatu kushoto) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano, Dickson Senzi (wapili kushoto) wakiongea mfanyabiashara eneo la Mwenge wakati wa ziara ya kutembelea wafanyabishara na kuangalia jinsi ya kupokea malipo kupitia LIPA SIMPO ya benki hiyo na kusisitiza kasi, usalama na gharama nafuu ya suluhisho za malipo ya kidijitali za Stanbic kwa biashara za ndani.
Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam, Februari 24, 2026 — Benki ya Stanbic Bank Tanzania imezindua rasmi huduma ya Lipa Simpo kwa wateja wake, hatua inayolenga kurahisisha malipo ya bidhaa na huduma kupitia simu bila kutumia fedha taslimu.
Huduma hiyo inaruhusu wateja kufanya malipo moja kwa moja kupitia Stanbic App au kwa kutumia USSD 15029#, huku wafanyabiashara wakiendelea kupokea malipo kupitia mfumo wa QR kutoka benki na mitandao yote nchini.
Akizungumza katika ziara ya kutoa elimu kwa wateja eneo la Mwenge, Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa benki hiyo, Edward Balandya, alisema huduma hiyo inalenga kufanya malipo kuwa ya haraka, salama na rahisi zaidi.
Aliongeza kuwa hadi Aprili 2026, miamala ya zaidi ya shilingi 40,000 itatozwa ada ya shilingi 1,000 tu, hatua inayokusudia kuwahamasisha wateja kutumia zaidi malipo ya kidijitali.
Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Dickson Senzi, alisema matumizi ya malipo yasiyo ya fedha taslimu yanaongeza uwazi wa biashara, hupunguza hatari za upotevu wa fedha na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.
Alisema kampeni za uhamasishaji zinazoendelea katika maeneo ya biashara nchini zinalenga kuonyesha matumizi halisi ya malipo kwa QR Code pamoja na kukusanya mrejesho kutoka kwa watumiaji wa huduma hiyo.
Kwa kuimarisha huduma za mawakala, malipo ya QR Code na gharama nafuu za miamala, Stanbic Bank Tanzania inaendelea kujiweka katika nafasi ya kuongoza mageuzi ya huduma za kifedha kidijitali nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: