Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC Philip Besiimire ( wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Vodacom jijini Dodoma, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kampuni hiyo karibu na wateja wa jiji hilo. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa kanda ya kati, Chiha Nchimbi (wa pili kulia) pamoja na Mdau wa Vodacom Emmanuel Makaki ( Kushoto) jana jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa watoa huduma wa duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma baada ya kulizindua jana. Kulia ni Mdau wa Vodacom, Emmanuel Makaki, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati, Chia Nchimbi (kulia kwake) na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (kushoto) akitazama moja ya simu zinazouzwa ndani ya duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma baada ya kulizindua jana. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa duka hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (wa pili kushoto) akitazama bidhaa zilizopo ndani ya duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma jana baada ya kulizindua. Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati, Chia Nchimbi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (wa pili kushoto) akizungumza na mtoa huduma wa dawati la wateja wenye mahitaji maalumu, Miraji Msita (kulia) baada ya kuzindua duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma jana. Kushoto kwake ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati, Chia Nchimbi, Mdau wa Vodacom, Emmanuel Makaki (kulia) na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, amezindua rasmi duka kubwa jipya la mfano mkoani Dodoma, hatua inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wateja wa mkoa huo pamoja na mikoa mingine ya Kanda ya Kati.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Besiimire amesema duka hilo ni mkombozi kwa wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kutokana na kuboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa huduma zake. Ameeleza kuwa duka hilo limezingatia mahitaji ya makundi mbalimbali ya wateja, ikiwemo huduma maalum kwa watu wenye mahitaji maalumu kama vile viziwi, wenye ulemavu wa miguu na macho, hatua inayodhihirisha dhamira ya Vodacom ya kutoa huduma jumuishi kwa kila Mtanzania.

Ameongeza kuwa ufunguzi wa duka hilo ni sehemu ya mkakati wa Vodacom wa kuwekeza katika uzoefu wa mteja (customer experience), kwa kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa haraka, kwa urahisi na kwa viwango vya juu zaidi kuliko ilivyokuwa awali.

Kwa upande wao, wateja wa Vodacom wameipongeza kampuni hiyo kwa uzinduzi wa duka hilo, wakisema kuwa hatua hiyo itawawezesha kupata huduma bora zaidi kutokana na maboresho yaliyofanyika, ikiwemo ukubwa wa duka, mazingira rafiki kwa wateja na upatikanaji wa huduma nyingi kwa sehemu moja. Wamesema duka hilo jipya linaonesha dhamira ya Vodacom ya kweli ya kujali wateja wake na kusogeza huduma karibu na jamii.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: