
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UDP, Saumu Rashid, akiwa na Mgombea mwenzi wa , Salim, Juma Khamis Faki,wakiwa wamenyanyua mikono juu kuashiria ushindi walioupata kwa kuchaguliwa kugombea nafasi ya Urais kupitia chama cha UDP.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UDP, Saumu Rashid akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya Chama hicho.
Na Mwandishi Wetu.
DAR ES SALAAM – Chama cha United Democratic Party (UDP) kimetangaza rasmi wagombea wake kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kikiwajumuisha Saumu Rashid (Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Juma Khamis Faki (Mgombea Mwenza), na Naima Salim Hamad (Urais wa Zanzibar).
Tangazo hilo limetolewa katika Mkutano Maalum wa UDP uliofanyika jijini Dar es Salaam, ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 390 kutoka mikoa 30 ya Tanzania Bara na Visiwani. Saumu Rashid alipata ushindi mkubwa kwa kura 376 za ndiyo dhidi ya kura 14 za hapana, akithibitishwa rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, aliwataka wagombea wake kushirikiana bega kwa bega wakati wa kampeni, akisisitiza ujumbe wa upendo na mshikamano badala ya chuki, ili kulinda amani ya taifa.
“Nchi hii ni yetu, hatuna pa kukimbilia. Tanzania ndiyo kwetu. Tuiweke salama na tuendelee kuienzi amani yake. Chama ni watu; bila watu hakuna chama,” alisema Cheyo.
Kwa upande wake, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sist Nyahonza, aliwapongeza wajumbe wa UDP kwa kuendeleza demokrasia kwa njia ya amani. Alisisitiza kuwa demokrasia ni kuheshimu sheria na taratibu, na kuwataka Watanzania kudumisha utulivu kipindi chote cha uchaguzi.
UDP itashiriki uchaguzi mkuu kwa kaulimbiu: “Imarisha Demokrasia, Tunza Amani.”


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments: