Wananchi wa kijiji cha CHEKERELI Kata ya Mabilioni Wilayani Sam,Mkoani Kilimanjaro, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 30 ambapo kutokana na ukosefu huu, wamekuwa wakilazimika kutumia maji ya Mto Ruvu kwa mahitaji yao ya kila siku, hali ambayo imechangia ongezeko la magonjwa ya tumbo na mengine yanayosababishwa na matumizi ya maji machafu.
Wananchi kijiji cha Chekereli LENI KIVUNGE na SILVANO HUSSEIN Wakizungumza kijijini hapo walieleza changamoto wanazokabiliana nazo.
"Tunatembea umbali wa kilomita tano kila siku kufuata maji ya mto tunalazimika kutumia maji haya kwa kunywa, kupika, na shughuli nyingine licha ya kujua yanaweza kuwa na madhara kwa afya zetu," alisema Leni
Wananchi hao wameeleza kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha mzigo mkubwa, hususan kwa wanawake na watoto ambao ndio hufanya kazi ya kuchota maji.
Aidha, wameeleza kuwa hali hiyo imeathiri maendeleo yao kwani muda mwingi hutumika kutafuta maji badala ya kushiriki shughuli za kiuchumi.
Akizungumzia kadhia hiyo Silvano amesema wao wamekuwa wakitumia maji hayo ambayo sia safi wala salama ambayo yamekuwa yakibeba takataka nyingi ambazo ni hatari kwa Maisha yao.
“Kwa hiyo tunaomba mbunge atusaidie sana ikiwezekana atutembelee kijijini kwetu aone na tumpe mawazo yetu ili aweze kutusidia tuondokane na changamoto hii’Alisema Silvano
Mbunge wa Same Magharibi almaarufu “mwana wa Kaya”akiwa katika ziara ya kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 aliyoipa jina la Operesheni Ahadi, amesikia kilio hicho na kutoa msaada wa mabomba 25 kwa ajili ya kusambaza kijijini hapo ili kuwasaidia kupunguza umbali wa kufuata maji.
"Sasa Chekereli ninawapatia roller za maji 25 kwa ajili ya kusambazia maji wananchi wangu wapate maji kule kwa sababu nao wamenipa kura mimi mbunge ili ikifika 2025 wakija hapa wakisema ntafanya hivi vile watakuta Mathayo keshafanya" alisema Mathayo.
Mathayo amesema anajua kuwa wananchi wa eneo hilo walikuwa wakipata shida kubwa ya maji hivyo mradi huo utakapokamilika utasaidia kusambaza maji katika eneo la Chekereli na wakina mama itasaidia kuwatua ndoo kichwani ili wasihangaike sana kwa sababu wamezaa mtoto wa kiume anaitwa Mathayo.
Wananchi wameishukuru mbunge Mathayo kwa hatua hiyo ya awali, lakini wamesisitiza haja ya kutekelezwa kwa mradi wa maji safi haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha yao na kuboresha hali ya maisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: