Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) katika mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Sehemu ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakiwa kwenye maandamano yaliyofanyika nje ya Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa neno la utangulizi kwa wahitimu wa kozi mbalimbali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wahitimu hao wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Sehemu ya Wahitimu wa Astashahada, Stashahada na Shahada ya kozi mbalimbali wakiwa wamesimama baada ya kutambulishwa kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) kabla ya Waziri huyo kuzungumza nao kwenye mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho akiwasilisha taarifa ya utendaji wa chuo kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa kofia nyekundu) akijumuika kwenye maandamano yaliyofanyika nje ya Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho Dkt. Dkt. Frolens Turuka.
Sehemu ya Wahitimu wa Astashahada, Stashahada na Shahada ya kozi mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa kofia nyekundu) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania waliofanya vizuri wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. Wengine ni Viongozi na Watendaji mbalimbali
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akicheza nyimbo ya kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania iliyokuwa ikizungumzia utendaji kazi mzuri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Vijana wa kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakitumbuiza kwenye mahafali ya 40 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.


Na Mwandishi Wetu _Mbeya


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewaasa wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kutumia vyema taaluma na ujuzi waliopata kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo katika sherehe za Mahafali ya 40 ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

“Kuhitimu ngazi za Shahada, Stashahada, Astashahada na Astashahada ya Awali katika fani mbalimbali sio jambo dogo, elimu mliyopata ni kubwa, tumieni elimu hiyo kwa manufaa yenu na ustawi wa taifa alisema Mhe. Simbachawene.

Aliongeza kuwa, ukuaji wa taifa lolote unategemea uwepo wa rasilimaliwatu imara na yenye weledi wa kutosha. Hivyo, amewataka wahitimu hao, kuepuka rushwa, ufisadi na kujikinga na ugonjwa hatari wa UKIMWI na magonjwa mengine yasiyoambuza kwa kuwa Taifa linawahitaji kwa ustawi imara.

Ameongeza kuwa, kuhitimu katika fani yoyote ile ni matokeo ya jitihada za muda mrefu si kwa wahitimu wenyewe tu bali pia hata kwa wale waliowasaidia kufikia hatua hiyo ikiwa ni pamoja na walimu, wazazi na walezi.

Vilevile, ameueleza Uongozi wa chuo kutambua kuwa Serikali ina matarajio makubwa na Chuo hicho hasa katika kuwajengea uwezo watumishi wa Umma na kutoa wahitimu wenye umahiri, uzalendo na tabia njema na hivyo kujenga uchumi wa nchi endelevu.

Awali, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Ernest Mabonesho alimshukuru Mhe. Simbachawene kwa kukubali mwaliko wao na kumtarifu kuwa pamoja na jitihada nyingine zinazofanywa na chuo pia, chuo kimeendelea na juhudi za kufufua na kuanzisha ushirikiano na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuboresha ujuzi na kubadilishana uzoefu.

Ili kuboresha mafunzo yetu, tumeona hainabudi kushirikiana na vyuo vingine vya nje na ndani ya nchi hususani vinavyohusika na masuala ya Utumishi wa Umma ili kuweza kupata fursa ya kujifunza na kutoa mafunzo bora zaidi alisema Dkt. Mabonesho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: