Na Mwandishi Wetu.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu ili sekta ya Biashara iwe na ushindani wenye viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Waziri Jafo ameyasema hayo katika Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani Duani yaliyofanyika leo Disemba 5, 2024 Jijini Dar es Salaam huku akitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wizara hiyo kushughulikia changamoto zote zinazowakabili wafanyabiashara.

Amesema lengo ni kuendelea kusaidia uwekezaji ili uende kwa haraka, na kuzitaka kampuni nchini kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji na kujihepusha kufanya udanganyifu

“Mijadala yote itakayojadiliwa katika maadhimisho hayo iwasilishwe kwangu ndani ya wiki mbili kwa lengo la kuhakikisha tunafanyia kazi mawazo yaliyojadiliwa.Tunataka kuongeza kasi katika kushughulikia changamoto zote zitakazoibuliwa na wadau wakati wa majadiliano.”

Awali Mwenyekiti wa Tume ya FCC Dkt Aggrey Mlimuka ameeleza kwamba tume hiyo pamoja na mambo mengine inawajibu wa kusimamia uwepo wa fursa sawa kwa washindani wakubwa na wadogo katika soko.

Pia tume hiyo ina jukumu la kupunguza ukiritimba katika masoko kwa kuhakikisha washindani wakubwa hawazuii washindani wadogo kukua na kuingia au kuwatoa sokoni.

Kwa upande wake William Erio ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa FCC, amesema kwamba maadhimisho hayo ya siku ya ushindani Duniani ni ya kwanza tangu kufanyika kwa marekebisho ya sheria nchini.

Ametoa shukrani kwa Rais samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge kwa kufanikisha kupitishwa kwa marekebisho na kuwa sheria jambo ambalo litatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa Desemba 5 ya mwaka Dunia huadhimisha siku ya ushindani na kwa Tanzania yamefanyika jijini Dar es salaam .Kauli mbiu ya katika maadhimisho hayo kwa mwaka huu inasema Sera ya Ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi.

“Wakati leo tunaadhamisha Siku ya Ushindani Duniani naomba kutumia nafasi hii kutoa shukrani kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson kwa kufanikisha kupitishwa kwa marekebisho na kuwa sheria.”
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza leo Disemba 5, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Ushindani Duniani ambayo yamebeba kauli mbiu “Sera ya ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi”

Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Ushindani (FCC) Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumza jambo leo Disemba 5, 2024 jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Ushindani Duniani ambayo yamebeba kauli mbiu “Sera ya ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi”
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio akizungumza jambo leo Disemba 5, 2024 jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Ushindani Duniani ambayo yamebeba kauli mbiu “Sera ya ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi”
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV





Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: