Akizungumza leo Aprili 23, 2024 katika Uzinduzi wa app mpya ya VTV ambapo ndani yake unaweza kustream tamthilia mpya kabisa ya EZRA inayoandaliwa na kampuni ya Lamata Village entertainment, Lamata amesema kuwa tamthilia EZRA ndani yake kuna visa na mikasa, story ya aina yake ambayo itawaacha watazamaji na wasikilizaji mdomo wazi huku ukitaka kujua yaliyojiri.Pia alitoa shukrani zake za kipekee kwa Uongozi wa Bodi ya Filamu kwa kushirikiana nao katika uzinduzi huo, huku akiwamwagia maua ya pekee kwa Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuweza kuwashika mkono na kufanikisha kazi hiyo.
Mshehereshaji Bw. Evance Bukuku akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa Tamthilia ya EZRA na app ya VTV.
Kwa upande wao Vodacom Tanzania wamewaalika watazamaji kuweza kupakua app ya VTV ili kuweza kuiona tamthilia hiyo kidijitali zaidi.
Usibaki nyuma! pakua app ya VTV leo google play au Appstore ufaidi mchapo mzima wa Ezra na burudani nyingine mbalimbali.
















Toa Maoni Yako:
0 comments: